Hatimaye ule mpambano wa kihistoria wa masumbwi uliosubiriwa kwa miaka mitano kati ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao unafanyika Mei 2 mwaka huu ndani ya MGM Grand in Las Vegas.
Ni pambano tajiri zaidi kutokea katika historia ya soka ambalo thamani yake inatajwa kuwa ni dola za Kimarekani milioni 250 huku Mayweather akirajiwa kutia kibindoni dola milioni 150 na Pacquiao akichukua dola milioni 100.
Mayweather, 37 bingwa wa dunia wa WBA na WBC, anajivunia rekodi yake ya kucheza michezo 47 bila kushindwa wakati Pacquiao, 36 bingwa wa WBO amecheza michezo 64 na kushindwa mara tano.
Mayweather amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo baada ya kuweka hadharini kupitia mitandao ya kijamii mkataba wa mtanange huo uliosainiwa na mabondia wote wawili.
Comments
Post a Comment