Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Wawakirishi wa Tanzania bara katika michuano ya Kombe la Shirikishi barani Afrika, Dar es salaam Young Africans wamefanikiwa kusonga mbele licha ya kuambulia kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa wenyeji wao BDF XI ya Botswana.
Dakika ya 3 Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa anakosa bao la wazi baada ya kubaki nna kipa lakini anapiga mpira ambao unatoka nje licha yakuwa Kipa na mabeki wa BDF XI kuwa chini.
Dakika ya 13 Simon Msuva anapiga kona lakini inakuwa haina matunda
BDF XI wanapata kupiga shuti kali ambalo linatoka nje na kuwa halina madhara kwa Yanga ikiwa ni dakika ya 14,
Dan Mrwanda anapata nafasi ambapo anapiga shuti kali ambalo linakuwa halina faida kwa Yanga kwani linatoka juu ikiwa ni dakika ya 15.
Simon Msuva anafanyiwa madhambi baada ya kuganyagwa mguuni na Mchezaji wa BDF XI kunako dakika ya 21, Muamuzi wa mchezo huo akaamua kutoa adhabu ya kadi Nyekundu kwa Mbotswana huyo.
Dakika ya 26 BDF wanapata faulo ya kwanza nje kidogo ya 18 ya Yanga ambapo inapigwa lakini inakuwa haina macho baada ya mabeki wa Yanga kuwa makini na kuondoa hatari hiyo.
Dan Mrwanda anapewa kadi ya Njano baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa BDF XI
Ngassa anaifungia Yanga bao la kichwa kufatia Simon Msuva ku chonga krosi ambayo inawabaatiza mabeki wa BDF na kumkuta Ngassa ambaye anapiga kichwa cha kuogelea.
Dakika ya 38 Kipa wa Yanga Aly Mustafa anagumbana na dhahama baada ya kuganyagwa mguuni na mshambuliaji wa BDF XI aliporudishiwa mpira ndio akagongana na mshambuliaji huyo katika mguu wa kulia.
Simon Msuva kwa mara nyingine anamimina kroi safi kutoka winga ya kulia ambayo inamkuta moja kwa moja kipa wa BDF XI ambaye anaidaka na kusaidia timu yake isizidi kuzama.
Dakika ya 45+2 kipindi cha kwanza Amis Tambwe anakosa bao baada ya kupiga kichwa ambapo mpira unagonga mwamba wa juu na kutoka baada ya Dan Mrwanda kuchonga krosi akitokea winga ya kushoto.
Hadi Mwamuzi wa mchezo huo kutoka Afrika KUsini anapuliza kipenga kuashiria kipindi cha kwanza kimemalizika Yanga walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 kutoka kwa Ngassa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa timu zote zikisaka mabao ndipo wenyeji hao BDF wakafanikiwa kusawazisha na kufanya kuwa 1-1.
Dakika ya 72 Dan Mranda anapewa kadi nyekundu kufatia kupewa kadi ya pili ya njano baada ya kumfanyia madhambi mchezaji wa BDF XI.
Dakika ya 75 BDF wanakosa bao baada ya gonga gonga lakini zinaishia kwa Aly Mustafa baada ya kudaka mpira wa kichwa cha mshambuliaji wa BDF XI.
Oscar Jushua anapewa kadi ya njano katika dakika ya 83 baada ya kuchelewesha muda kwa kuchelewa kurusha.
BDF XI wanapata bao la pili kupitia kwa Madziba katika dakika ya 85 Baada ya mchezaji huyo kupiga kichwa ambacho kinagonga mwamba na kurudi ndani na kumkuta tena naambapo anaupiga kwa mguu na kutumbukia kimiani.
Hadi mwamuzi wa mtanange huo anamaliza mchezo Yanga walikuwa nyuma kwa bao 2-1 lakini wanakuwa wamevuka katika hatua hiyo kwa jumla ya goli 3-1.
Comments
Post a Comment