Muda wa kuonesha vipaji NSSF-Real Madrid Sports Academy wawadia!


Muda wa kuonesha vipaji NSSF-Real Madrid Sports Academy wawadia!

IMG_0122 (1)

NSSF_Real Madrid Sports Academy.

Baada ya uandikishaji kwaajili ya kufuzu kujiunga na NSSF_Real Madrid Sports Academy. Awamu inayofuata ni ya majaribio ambayo itafanyika Jumamosi tarehe 28 Februari 2015 kwenye viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12:45 asubuhi. Majina ya vijana watakao hudhulia awamu hii yamechapishwa kwenye magazeti ya  Mwananchi, Majira na Mtanzania leo tarehe 27 Februari 2015.

 Majina ya vijana watakao hudhulia majaribio ya awamu nyingine yatachapishwa kwenye magazeti ya wiki ijayo.

 Kwa wale walio orodheshwa wanaombwa kufika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza majaribio.

Pia wazazi au walezi wanaombwa waambatane na watoto wao wakiwa wamewapatia vifaa vya michezo kama vile viatu,soksi, Shin guard, kaptula na flana ya michezo, maji na gharama za usafiri wajitegemee.



Comments