Mtukutu Barton aomba msamaha


Mtukutu Barton aomba msamaha

25E908BB00000578-0-image-a-10_1424534519615

Na Augustino Mabalwe

Nahodha wa klabu ya Qpr Joe Barton ameomba msamaha kwa wachezaji na mashabiki wa timu hiyo mara baada ya hapo jana kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo waliofungwa 2-1 na hull City katika uwanja wa KC.

Mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle United alipewa kadi hiyo dakika ya 32 ya mchezo baada ya kumsukuma mchezaji wa hull city Alex Bruce na pia kuonesha nia ya kutaka kumpiga kiungo Tom Huddlestone

Tukio hili lilitokea wakati Joe Barton akijaribu kumtetea kinda wa timu yake Darnell Fullong baada wachezaji wa Hull City kumtaka mwamuzi Anthony Taylor ampe kadi kinda huyo kwa kosa la kumchezea vibaya kiungo David Meyler.

Baada ya mchezo huo kumalizika Joe Barton alisema kuwa ni jukumu lake yeye kama nahodha kuwalinda wachezaji wa timu yake.

"Ninaomba msamaha kwa wachezaji wenzangu na kwa mashabiki wote mliosafiri kuja hapa leo " Alisema

Hii ni kadi nyekundu ya saba katika maisha ya soka ya mchezaji huyo anayefahamika kwa utukutu duniani.

Matokeo hayo yanaifanya Qpr kushika na nafasi ya 17 ikiwa na pointi 22 na mechi ijayo wanakibarua kizito watakapokutana na Arsenal na siku chache baadaye watawavaa Tottenham Hotspur.



Comments