‘MRITHI’ WA KANUMBA ASEMA ANAKUJA KIVINGINE …ni Philemon Lutwaza aliyem-copy Kanumba katika “After Death”



'MRITHI' WA KANUMBA ASEMA ANAKUJA KIVINGINE …ni Philemon Lutwaza aliyem-copy Kanumba katika "After Death"
'MRITHI' WA KANUMBA ASEMA ANAKUJA KIVINGINE …ni Philemon            Lutwaza aliyem-copy Kanumba katika

MWIGIZAJI aliyejizolea umaarufu katika filamu ya "After Death" Philemon Lutwaza 'Lutwaza' (pichani juu) anayefananishwa zaidi na marehemu Kanumba, amesema yeye ni mkongwe katika game kwani alianza kuigiza toka enzi ya Fukuto Arts Professional chini ya Mr. Chuzi.

Lutwaza ameshiriki katika tamthilia kibao zilizoandaliwa na Tuesday Entertainment kama vile Milosis, Jasmini huku filamu yake ya kwanza kucheza ikiwa ni "Bad Night" ya mwaka 2007 iliyotayarishwa na Kitale.

"Ni kweli naweza kusema kuwa jina langu limejulikana sana baada ya kucheza filamu ya After Death lakini mimi ni mkongwe kwenye game nimeanza kuigiza mwaka 1999, na nimefanya kazi nyingi," anaeleza Lutwaza.

"Na sasa ili kudhihirisha uwezo wangu, nakuja na filamu yangu mwenyewe iitwayo Anko Kiepe," anaongeza msanii huyo na kufafanua kuwa ni kazi nzuri ambayo kwa mara nyingine watu watamuona Lutwaza akifanya maajabu katika tasnia filamu Bongo.

Kwa mujibu wa Lutwaza, filamu ya Anko Kiepe imekamilika na inatarajia kuingia sokoni wakati wowote baada ya taratibu za usambazaji kukamilika.

Habari kwa hisani ya FilamuCentral.



Comments