MONACO YAIFYATUA ARSENAL 3-1 EMIRATES, WENGER ALAUMU ‘DEFENCE’ YAKE … Bayer Leverkusen yaichapa Atletico Madrid 1-0
Arsenal ina mlima mrefu wa kupanda kama kweli inataka kupenya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Hiyo ni baada ya kukubali kipigo cha bao 3-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani (Emirates) kutoka kwa Monaco ya Ufaransa.
Hadi mapumziko Monaco ilikuwa mbele 1-0 kwa goli lililofungwa na Geoffrey Kondogbia katika dakika ya 38.
Shuti la Kondogbia likambabatiza Per Mertesacker na kumpoteza maboya kipa David Ospina kabla mpira haujatinga wavuni.
Katika kipindi cha kwanza Arsenal haikufanikiwa kupiga hata shuti moja lililolenga goli
Dimitar Berbatov akarejea vizuri kwenye ardhi ya England baada ya kuifungia Monaco bao la pili iliopotimu dakika ya 53.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Spurs, Manchester United na Fulham alifunga bao hilo baada ya shambulizi la kushtukiza huku akiwa amezongwa na wachezaji watatu wa Arsenal.
Mchezaji aliyetokea benchi Alex Oxlade-Chamberlain akaifungia Arsenal bao pekee katika dakika za mareruhi (90+1) na kurejesha matumani kwa wenyejeji.
Lakini Arsenal ikafanya makosa katika sekunde za mwisho kabisa za mchezo (90+4) kwa kuacha lango wazi huku wachezaji wengi wakienda mbele kutafuta bao la kusawazisha na kutoa mwanya kwa Yannick Ferreira-Carrasco kuifungia Monaco goli la tatu.
Kocha Arsene Wenger ameishutumu vikali safu yake ya ulinzi na kukiri kuwa haikucheza vizuri.
Goli la tatu ndilo lililomkera zaidi Wenger: "Ukiwa 2-1 ukingoni kabisa mwa mwa mchezo unaacha vipi eneo lako la ulinzi wazi?" alihoji kocha huyo wa Arsenal.
Hata hivyo Wenger amesema ingawa wana mlima mrefu wa kupanda, lakini bado hawajakata tama ya kusonga mbele.
Arsenal 4-2-3-1: Ospina 7, Bellerin 4.5, Mertesacker 4.5, Koscielny 5, Gibbs 5, Coquelin 4.5 (Oxlade-Chamberlain 68, 7), Cazorla 5 (Rosicky 82), Sanchez 6, Ozil 4.5, Welbeck 5, Giroud 4 (Walcott 60, 6). Subs not used: Szczesny, Gabriel, Monreal, Chambers.
Monaco 4-1-4-1: Subasic 7, Toure 7.5, Wallace Santos 8.5, Abdennour 8, Echiejile 7.5, Dirar (Kurzawa 82), Kondogbia 8, Fabinho 7, Joao Moutinho 9, Martial 8 (Bernardo Silva 84), Berbatov 8 (Ferreira-Carrasco 76, 8). Subs not used: Stekelenburg, Matheus Carvalho, Alain Traore, Diallo.
Katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa Bayer Leverkusen ikiwa nyumbani iliifunga Atletico Madrid 1-0 kupitia kwa Hakan Calhanoglu.
Comments
Post a Comment