Kiungo mkongwe wa Manchester United Michael Carrick anajiandaa kusaini mkataba mpya wa miezi 12 klabuni hapo.
Carrick amekuwa 'mwanachama' muhimu kwenye kikosi cha Louis van Gaal baada ya kurejea dimbani mwezi Novemba kutoka kwenye kuuguza maumivu ya muda mrefu ya kifundo cha mguu.
Hata hivyo kiungo huyo yuko tena nje ya dimba safari hii ikiwani ni waumivu ya msuli lakini bado United inaona ni jambo sahihi kumwongeza mkataba.
Carrick, 33 ambaye analipwa pauni 130,000 kwa wiki, amesema mipango yake ni kuendelea kuitumikia United pindi atakapomaliza mkataba wake wa sasa unaomalizika mwezi Juni.
Van Gaal na Ryan Giggs wote ni mashabiki wa kiungo huyo mkongwe na wanatarajiwa kuhamasisha kukamilika kwa dili hilo mapema iwezekanavyo.
Comments
Post a Comment