Mchawi wa Simba kujulikana kesho Mkutanoni



Mchawi wa Simba kujulikana kesho Mkutanoni

Wanachama-1Na, Richard Bakana, Dar es salaam

Uongozi wa klabu ya Simba pamoja na wanachama, kesho jumapili Machi 1, wanatarajia kukutana katika mkutano wa klabu unaotambuliwa na katiba ya Mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara, ili kujadiri maswala yanayo ihusu timu hiyo.

Mkutano huo ambao ulikuwa ufanyike toka mwezi Desemba 2014 ikashindikana kutokana mambo kuingiliana, sasa utafanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kusawazisha matatizo yaliyopo kwenye klabu hiyo.

Akiongea na Shaffihdauda.com Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva amesema kuwa mkutano huo utakuwa na ajenda moja tu 'Kujadiri mwenendo wa timu katika mbio za ligi kuu' ambapo unatarajia kuanza majira ya saa nne asubuhi.

Leo jioni Simba SC watakuwa katika kibarua kizito katika Uwanja wa Taifa ambapo watakuwa wakiminyana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.



Comments