MASHAUZI CLASSIC KUPELEKA SURA SURAMBI DODOMA JUMAMOSI HII …Ijumaa wapo Kibaigwa, Jumapili Chalinze



MASHAUZI CLASSIC KUPELEKA SURA SURAMBI DODOMA JUMAMOSI HII …Ijumaa wapo Kibaigwa, Jumapili Chalinze
MASHAUZI CLASSIC KUPELEKA SURA SURAMBI DODOMA JUMAMOSI            HII …Ijumaa wapo Kibaigwa, Jumapili Chalinze

Wakazi wa Dodoma Jumamosi hii watakuwa na fursa ya kula raha za kundi la Mashauzi Classic huku kubwa zaidi likiwa ni utambulisho wa nyimbo mpya ikiwemo "Sura Surambi".

Likiwa Dodoma mjini, kundi hilo litatumbuiza katika ukumbi mpya na wa kisasa - Shangilila Perugina Club.

Mkurugenzi wa kundi hilo Isha Mashauzi ameiamba Saluti5 kuwa Ijumaa (siku moja kabla ya onyesho la Dodoma), watafanya onyesho lingine kwenye mji wa Kibaigwa ndani ya ukumbi wa Maisha Plus na watakapokuwa njiani kurejea Dar es Salaam, watatumbuiza Chalinze kwenye ukumbi wa Ndelema Inn Jumapili hii.

Mkurugenzi huyo amesema katika maonyesho hayo matatu, watatambulisha nyimbo  mpya kabisa "Ubaya Haulipizwi" wa Asia Mzinga, "Tuacheni Tulale" wa Hashim Said, "Mapenzi Yamenivuruga" wa Naima Mohamed pamoja na songi linalokimbiza kwa sana "Sura Surambi" wa kwake Isha Mashauzi.

Aidha, Isha amesema pia katika maonyesho hayo atatambulisha nyimbo zake za nje ya taarab "Nimlaumu Nani" uliopigwa katika miondoko ya rhumba, "Nimpe Nani" (Zouk Rhumba) na "Ado Ado" wa mchiriku.



Comments