Mwimbaji nyota wa Mashauzi Classic, Saida Ramadhan maarufu kama Saida Mashauzi, amejifungua mtoto wa kike leo asubuhi.
Saida ambaye ni mdogo wake na Isha Mashauzi amekuwa nje ya jukwaa la kundi hilo kwa zaidi ya miezi mitano.
Akiongea na Saluti5, Saida ambaye anatamba na wimbo "Ropekeni Yanayowahusu" amesema anamshukuru Mungu amejifungua salama katika hospitali ya Mwananyamala asubuhi ya saa 4 kasorobo.
Tupia macho picha kadhaa za Saida Mashauzi na mwanae.
Mtoto wa Saida Mashauzi
Akiwa na afya tele
Akiwa amepakatwa na mama yake
Nani Kama Mama?
Saida Mashauzi na mwanae na mwanae
Tabasamu la mama
Saida akiendelea kula 'raha' za malezi ya mtoto
Utulivu makini
Mtu na mama yake
Mola ampe afya njema na umri mrefu
Comments
Post a Comment