MASHABIKI WA YANGA WALIVYOITEKA MBEYA …ni shangwe za kufa mtu kuelekea Sokoine Stadium ...Mbeya City yalala 3-1
Mashabiki Yanga wamegubiga shangwe za aina yake jijini Mbeya kuelekea mchezo wa Ligi Kuu wa timu yao na wenyeji Mbeya City.
Mechi hiyo ikapigwa katika uwanja wa Sokoine huku tambo na mbwembwe za aina yake zikitawala kutoka kwa mashabiki wa Yanga, wengi wao wakiwa wametoka Dar es Salaam, kabla na baada ya mechi.
Katika mchezo huo Yanga ikashinda 3-1 na kuzidi kujitanua kileleni mwa msimamo wa ligi.
Tupia picha kadhaa zilizopigwa kabla ya mechi hiyo na mdau wetu Engi Muro Mwanamachame ambaye nae yuko jijini Mbeya kushuhudia pambano hilo la aina yake.
Safari ya kuelekea Sokoine Stadium
Cheki mkwara huo!
Ni shangwe kwa kwenda mbele
Shangwe zinaendelea
Ni kama vile wana uhakika na ushindi
Si mchezo watu na timu zao bwana!
Comments
Post a Comment