Ijumaa iliyopita katika kuadhimisha mwaka mpya kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pale Mlimani City kulikuwa na burudani moja iliyoacha gumzo la aina yake.
Burudani hiyo ilitoka kwa bendi ya Mapacha Watatu ambao ndio walikuwa watoa burudani pekee katika tukio hilo.
Mapacha wakatoa burudani ya kufa mtu iliyowaacha hoi waalikwa wakiwemo wahadhiri na wafanyakazi wote wa UDSM pamoja na viongozi wa kitaifa waliowahi kupata elimu yao katika chuo hicho.
Bendi hiyo chini ya Jose Mara na Khalid Chokoraa, ilitumbuiza kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 4 za usiku.
Moja ya vivutia kutoka kwa Mapacha ilikuwa ni namna walivyoweza kupiga muziki wa kila kona ya dunia achilia mbali nyimbo zao wenyewe.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za Mapacha Watatu katika sherehe hizo.
Comments
Post a Comment