Sababu tisa (9) kwanini hili ni pambano la uzito wa juu kabisa ambalo litatikisa dunia. Hii ni baada ya Manny Pacquiao na Floyd Mayweather kuwa mbioni kuzichapa katika pambano la thamani zaidi ulimwenguni.
1. Pacquiao v Mayweather ni pambano ambalo dunia italishuhudia baada ya kulihitaji kwa kipindi kirefu.
Pacquiao ni bondia ambaye anajitolea kwa kiasi kikubwa ili kunusuru janga la umasikini katika taifa lake wakati Mayweather ni mtu aliyejitengennezea pesa kwa kiasi kikubwa kupitia masumbwi (zaidi ya dola za kimarekani million mia nne ($400 million). Hii inalifanya pambano hilo kulinganishwa na mapambano mengin ya kuvutia yalopita kama vile ilivyokuwa kwa Muhammad Ali v Joe Frazier, Jack Dempsey v Gene Tunney, Sugar Ray Robinson v Jake LaMotta. Ni wazi kukutana kwao kutatngeneza historia nyingine
2. Utengano katika historia zao umesababisha mvutano, mbinu mbali mbali, tamaduni na imani.
Mayweather amkuwa bingwa wa dunia kwa mara ya kwanza alipotwaa ubingwa wa uzito wa juu wa WBC mnamo mwaka 1998 na amekuwa akipata umaarufu kila uchao sawa na ilivyo kwa Manny Pacquiao ambaye alitwaa ubingwa wa (WBC flyweight champion) mwaka huo huo. Hiii inafanya pambano lao kuonekana kama lililotarajiwa siku moja
3. Pambano hili linampa fursa Mayweather kudhihirisha ya kuwa yeye ni mpambanaji bora katika dunia.
Mayweather hajapigwa, anasifika kwa kujihami ilihali Pacquiao ni mpambanaji mwenye vurugu na mwenye kutumia nguvu. Floyd anejivunia rekodi ya kushinda mapambano 47 bila kupoteza huku 26 kati ya hayo akiyashinda kwa knockout huku akijiita aliyebora zaidi (TBE). Hivyo ni wazi kama atashinda pambano hili basi atakuwa kaacha kumbukumbu katika ulimwengu wa masumbwi. Pacquiao, ye kwa upande wake ni bondia aliyejishindia mataji katika kanda nane tofauti kuanzia uzito wa juu mpaka ule wa kati akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 57 huku akipotza matano. Lakini kila anapopoteza amekuwa mwenye kurudi akiwa ameimarika zaidi. Hii inalifanya pambano hili kungojewa kwa hsauku kubwa kwani ni muda sasa Mayweather hajapata upinzani wa kutosha ulingoni na Pacquiao anaweza kuwa mtu sahihi katika hilo.
4. Ni pambano ambalo linabashiriwa kuvunja rekodi ya dunia ya masumbwi katika kila idara:
Ikumbukwa pambano linaloongoza kwa kuwa na kiingilio kikubwa (2.4 million buys) ilikuwa kati ya Mayweather na Oscar De La Hoya; pambano lililovuna apato zaidi ya $150 milioni ilikuwa kati ya Mayweather na Saúl Álvarez, wakati pamabno lililoongoza kwa mapato ya mlangoni pia mpaka sasa ($20milion) ni kati ya Mayweather na Álvarez. Hivyo inakadiriwa kuwa pambano hili linaweza likafikia robo bilioni ya dola la Kimarekani
5. Ni pambano ambalo wapambanaji watakuwa wamejiandaa kwa miaka sita (6).
Pambano hili la mwisho wa ubishi kati ya Mayweather na Pacquiao limekuwa likijadiliwa toka 2009. Hata likapangwa kufanyika mwezi Machi 13, 2010, kabla halijakwama baada ya mfilipino (Manny) kugombea vipimo vya utumizi wa madawa na hatimaye kuvunja mazungumzo.
6. Ni pambano ambalo litakuwa na mvuto hadi watu wengi mashuhuri kuhudhuria.
Kama namna ambavyo Mike Tyson alivyokuwa bondia aliyefanikiwa kuwavuta watu mashuhuri kila alipopigana au hata pambano la kihitoria linalojulikana kuwa la karne kati ya Muhammad Ali na Joe Frazier la mwaka 1971 huko Madison Square Garden, ambapo mpiga picha Frank Sinatra alikosa pa kukaa bais tegemea jambo kama hilo. Miongoni mwa mastaa wanaopenda ndondi kwa sasa ni pamoja na Jay Z, Sean Combs (P.Diddy), Mark Wahlberg na Jeremy Piven ambao mara kwa mara wametembelea LA Gym, The Wild Card, mahala ambapo Pacquiao anafanyia mazoezi.
Hapo hujawazungumzia nyota wengine kama Arnold Schwarzenegger na Sylvester Stallone 'Rambo" ambao ni kawaida kuwaona. Hivyo ni wazi tegema hali kama hiyo huku kukiwa na lundo la watu mashuhuri toka kwenye muziki, filamu na michezo mingine nje ya masumbwi.
7. Halitarajiwi kuwa miongoni mwa mapambano makubwa ya ndondi ambayo wapenzi wa masumbwi hawakushuhudia
Itakuwa fedheha kubwa endapo litakuwa pambano sawa na yale ya Jake LaMotta v Rocky Graziano, au Riddick Bowe v Lennox Lewis yalokosa kuvutia. Ni wazi hili litakuwa pambano la kukumbukwa kwani kama litashindwa kuendela kwa sababu yoyote basi litaharibu historia ya namna yoyote.
8. Umri wao
Ifikapo februari 24, Mayweather anatimiza miaka 38 wakati Pacquiao atakuwa na 37 ifikapo disemba
9. Ni historia
Hii inatokana na ukweli kwamba toka akiwa kijana mdogo Pacquiao alikuwa akipigana ili kuilisha familia yake akipeleka dola kadhaa kwa mama yake. Watu wa ufilipino wanampenda sana hasa ikizingatiwa pia ya kuwa ni mwanasiasa mashuhuri nchini mwao tofauti na Mayweather ambaye ambaye alijifunza ubondia toka akiwa shule. Nje ya ulingo ni nyota wa Pop anayependwa.
ITAENDELEA KESHO…..
Comments
Post a Comment