MANCHESTER UNITED YASONGA MBELE FA CUP …SASA KUVAANA NA ARSENAL ROBO FAINALI, DI MARIA NYOTA WA MCHEZO
Manchester United imepata ushindi mnono wa bao 3-1 dhidi ya timu ndogo ya Preston North End kwenye mechi ya FA Cup.
Hata hivyo United iliyokuwa ugenini, ililazimika kutoka nyuma na kupambana hadi kuibuka na ushindi huo mtamu.
Preston walitangulia kufunga dakika ya 48 kwa bao la Scott Laird lakini ilipotimu dakika ya 65 Ander Herrera akaisawazishia United baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Antonio Valencia.
Dakika ya 72 kwa mara nyingine tena Valencia akafanya kazi nzuri ya kuchanja mbuga wingi ya kulia na kutoa krosi tamu iliyomkuta Marouane Fellaini ambaye alipiga kichwa kilichopanguliwa na kipa Thorsten Stuckmann kabla ya nyota huyo wa Ubelgiji hajauwahi mpira na kuujaza wavuni.
Wayne Rooney akaifungia United bao la tatu kwa njia ya penalti dakika ya 88 na kuihakikishia timu yake nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali ambako sasa itavaana na mabingwa watetezi Arsenal kwenye dimba la Old Trafford.
Kwa mujibu wa ratiba ya robo fainali iliyotolewa masaa kadhaa yaliyopita, Arsenal ilikuwa inasubiri mshindi kati ya Preston na United huku Liverpool ikipangwa na Blackburn Rovers. Bradford itaumana na Reading wakati Aston Villa ikiikaribisha West Brom.
Katika mchezo wa United na Preston, mshambuliaji Angel Di Maria ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo ambapo alikuwa akiichambua ngome ya wenyeji vile alivyotaka.
Kwa mara nyingine tena Falcao alishindwa kung'ara
Scott Laird akishangilia bao lake dhidi ya United
Preston (3-4-1-2): Stuckmann 6; Humphrey 6.5, Huntington 7, Clarke 7, Wright 6 (Wiseman 75, 6); Welsh 6.5; Kilkenny 7 (Reid 75, 6), Gallagher 7, Laird 7.5; Davies 6.5 (Robinson 75, 6), Garner 7.
Manchester United (4-1-3-2): De Gea 5.5; Valencia 6.5, Smalling 5.5, Rojo 6, Shaw 6; Blind 7; Herrera 6.5, Fellaini 7, Di Maria 8; Rooney 6.5, Falcao 5 (Young 60, 6.5).
Comments
Post a Comment