Manchester United imerejesha makali yake kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga Sunderland 2-0 katika mchezo mkali uliopigwa Old Trafford.
Alikuwa ni mshambuliaji Wayne Rooney aliyewapa raha mashabiki wa United baada ya kufunga magoli yote mawili.
Hata hivyo United ilibidi isubiri hadi dakika ya 66 pale Rooney alipofunga kwa mkwaju wa penalti baada ya John O'shea kumchezea faulo Radamel Falcao.
Mwamuzi Roger East akafanya kituko kwa kumpa kadi nyekundu beki Wes Brown badala ya Jonh O'shea aliyecheza faulo hiyo.
Dakika ya 84 Rooney akafunga bao la pili kwa kichwa na kuzima matumaini ya Sunderland kusawazisha.
Manchester United: De Gea; Valencia, Smalling, Evans, Rojo, Blind; Herrera, Young, Di Maria (Januzaj); Rooney (Mata), Falcao (Fellaini)
Sunderland: Pantilimon; Reveillere, van Aanholt, Brown, O'Shea (c); Cattermole, Larsson, Gomez, Johnson (Fletcher); Wickham (Fletcher), Defoe (Fletcher).
Comments
Post a Comment