Mambo matano katika sera ya Figo FIFA



Mambo matano katika sera ya Figo FIFA

download

Nyota wa zamani, aliyepata pia kunyakua uchezaji bora wa dunia, Luis Figo ambaye ni mmoja wa wagombea wa uraisi wa kiti cha shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) akigombea sambamba na raisi wa sasa Sepp Blatter pamoja nao Michael van Praag na Prince Ali Bin Al Hussein amebainisha mambo muhimu atayoyapa kipaumbele akiwa Fifa

 Moja kati ya mambo anyokusudia kuyafanya gwiji wa soka Luis Figo Luis Figo endapo atachaguliwa kuwa raisi wa Fifa ni kuongeza idadi ya timu shiriki katika kombe la dunia sambamba na kubadili kanuni za adhabu ya kuotea (offside).

Nyota huyo wa zamani wa vilabu hasimu vya Real Madrid na Barcelona ni mmoja kati ya wagombea wa hatua ya fainali ya kumpata raisi wa sasa wa Fifa Sepp Blatter ambaye pia atatetea kiti chake hapo mwezi mei mwaka huu

 Mashabiki wengi wa soka wanasubiri kwa hamu kushuhudia nyuso mpya katika shirikisho hilo tofauti na utawala wa Blatter ambao umekumbwa na tuhuma na rushwa na kujuana. 

Nyota huyo toka Ureno amewataka wajumbe kuungana naye ili kuleta aina mpya ya uongozi Fifa, ambapo anakusudia kuwa na uongozi ambao utazingatia soka la ulimwengu na kulitetea. Miongoni mwa mambo alobainisha ni kama ifuatavyo;

  1. Kuongeza idadi ya timu shiriki Kombe la dunia

Endapo atachaguliwa Figo ambainisha kusudio lake la kuongeza idadi ya timu shiriki toka 32 za sasa mpaka 40 au pengine 48. Hii ina maana kuwa endapo fifa atakabidhiwa rungu basi michuano hiyo mikubwa kabisa ulimwenguni itagawanywa katika hatua mbili za awali ambayo inaweza kufanyika katika mabara tofauti kabla ya hatua ya fainali kufanyikia katika taifa moja. Kwa namna yoyote ni wazi timu shiriki zitaongezeka kwa mbara mengine. Hii siyo tu itasaidia kuongeza timu shiriki bali pia kukuza mapato ambayo yanaweza kutumika kukuza soka ulimwenguni.

  1. Kuwekeza nusu ya mapato ya Fifa katika soka la vijana kwa miaka minne

 Kwa mujibu wa Figo, fifa italazimika kutumia $2.5 bilioni (sawa na euro £1.62 bilion) ambayo ni karibu nusu ya mapato yake ili kukuza soka kuanzia ngazi za chini. Kwa mujibu wa mgombea figo hii itasaidia kuyaimarisha mashirikisho mbalimbali na hivyo kufanikisha kusudio la ujumla la kuimarisha soka kwa kiwango cha juu:

  1. Kuongeza utumizi wa Teknolojia

 Kwa mujibu wa Figo, Fifa lazima iendelee na utumizi wa teknolojia ya kutizama kama mpira umevuka mstari wa lango na si hivyo tu bali pia ianze mjadala wa uwezekano wa kuanza kutumia tecknolojia hasa katika soka. Kwa mujibu wa nyota huyo hatua hizo ni muhimu ili kuhakikisha soka linakuwa madhubuti kwa muda muafaka. Kanuni kama hizo pia zitasaidia kuepusha adhabu mara mbili kwa kosa moja kwa mchezaji, mfano mchezaji anapewa kadi nyekundu, penati inatolewa na kisha baadaye anasimamishwa tena kwa michezo hata mitatu. Hata hivyo Figo hajabainisha nini kifanyike katika hali hiyo.

  1. Uanzishwaji wa adhabu endapo mwamuzi atadhihakiwa au kuoneshwa tabia zisizostahili

Kwa mujibu wa Figo hili litafanyika ikiwa ni pamoja na kurejea kanuni ya zamani ya adhabu ya kuotea ambayo ilihusisha mchezaji kuhesabiwa kaibiwa pasipo kujali anahusika moja kwa moja au la.

  1. Mgawanyo wa pesa za Akiba za Fifa si sahihi

Kwa mujibu wa Figo badala ya kukalia pesa, fungu hilo litumike kugawiwa mashuleni na kuinua soka la vijana ili kuuborehsa mchezo wa mpira wa miguu ulimwenguni.



Comments