Luis Suarez ameendelea kuwa moto wa kuotea mbali anapokuwa kwenye eneo la goli baada ya kuifungia Barcelona bao moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Granada.
Barcelona ikiwa ugenini kwenye mchezo huo wa La Liga, ikawachukua dakika 26 tu kupata bao kuongoza kupitia kwa Ivan Rakitic na kufanya wageni waende mapumziko wakiwa mbele kwa 1-0.
Dakika chache baada ya mapumziko, Suarez akaifungia Barcelona bao la pili kabla ya Fran Rica kupunguza moja dakika ya 53.
Zikiwa zimesalia dakika 20, Lionel Messi akahitimisha ushindi wa Barcelona kwa kufunga bao la tatu akimalizia kazi nzuri ya Suarez.
Granada: Oier; Nyom, Babin, Cala, Foulquier; Iturra, Rico, Marquez (Rochina 67); Bangoura (Candeias 79), Ibanez. Cordoba (Isaac 78)
Barcelona: Bravo; Alves, Bartra, Mathieu (Busquets 75) , Alba; Mascherano, Xavi (Rafinha 65), Rakitic; Messi, Neymar.
Comments
Post a Comment