Southampton imepoteza nafasi ya kuishusha Manchester United kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kukubali kipigo cha bao 2-0 kutoka kwa Liverpool.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Southampton wakajikuta wakichapwa bao la mapema kunako dakika ya 3 kupitia kwa Coutinho.
Hali ikawa mbaya zaidi kwa wenyeji pale ilipotimu dakika ya 73 baada ya kukubali bao la pili lililofungwa na mshambuliaji hatari Raheem Sterling.
Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu uliochezwa Jumapili Everton ikiwa nyumbani ikalazimishwa sare ya 2-2 dhidi ya Leicester City.
Southampton: Forster, Clyne, Fonte, Yoshida, Targett, Ward-Prowse (Mane 57'), Wanyama, Steven Davis (Schneiderlin 46'), Elia Djuricic (Tadic 75'), Pelle
Liverpool: Mignolet, Can, Skrtel, Lovren, Ibe (Johnson 75'), Henderson, Allen, Markovic (Moreno 46'), Lallana (Sturridge 62'), Coutinho, Sterling
Comments
Post a Comment