Licha ya kufungwa Yanga yaitupa nje BDF XI


Licha ya kufungwa Yanga yaitupa nje BDF XI
1510863_889463071096227_1652913715140602198_n
YANGA SC wamefanikiwa kufuzu raundi inayofuata ya kombe la Shirikisho baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana kwa wastani wa mabao 3-2.
Wawakilishi hao wa Tanzania wamefungwa magoli 2-1 katika mechi ya marudiano iliyopigwa usiku huu uwanja wa Lobatse, mjini Gaborone, lakini wanafanikiwa kusonga mbele kutokana na faida ya ushindi wa mabao 2-0 walioupata februari 14 mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Bao la Yanga leo hii limfungwa na Mrisho Khalfan Ngassa 'Anko' katika dakika ya 29′ ya kipindi cha kwanza.
REPOTI YA MECHI
Yanga mabingwa mara 24 wa ligi kuu Tanzania bara walianza mchezo kwa kasi, wakigongeana pasi za uhakika.
Mapema dakika ya 3′ Mrisho Khalfan Ngassa aliyekuwa kwenye ubora wake alikosa nafasi nzuri ya kufunga goli la kuongoza kufuatia mabeki wa BDF XI kufanya uzembe.

BDF, mabingwa  mara 7 wa ligi kuu Botswana waliendelea kukalia kiti cha moto, lakini walifanya jaribio nzuri dakika ya 14′ na  shuti lililopigwa na mchezaji wa timu hiyo lilipaa sentimita chache langoni kwa Yanga.

Kiujumla dakika 15′ kipindi cha kwanza timu zote zilitengeneza mashambulizi ila Yanga walionekana kuwa katika ubora wa juu.

Dakika ya 18′ BDF walipata pigo baada ya mchezaji wao   Othusitse kuoneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumchezea rafu mbaya, Saimon Msuva wa Yanga.
Msuva alipata maumivu na kutolewa nje kwa muda kwa ajili ya matibabu kutokana na rafu hiyo, lakini dakika chache baadaye alirejea uwanjani tena.
Yanga wenye historia ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa mwaka 1998 walitumia mwanya wa Wanajeshi wa jeshi la ulinzi la Botswana (BDF) kuwa pungufu na kushambulia kama nyuki.
Dakika ya 29′ Msuva mwenye kasi dimbani aliingiza majalo safi kutoka upande wa kulia wa lango la BDF na mpira huo ulimkuta Amissi Tambwe aliyepiga pasi iliyokwenda kutua kichwani kwa Mrisho Ngassa na mjomba hakufanya makosa akaifungia Yanga goli la kuongoza.
Kuingia kwa bao hilo kuliwafanya Yanga watakate zaidi dimbani wakipasiana pasi nzuri na kutengeneza mashambuli. Wenyeji walionekana dhahiri kuhamanika.
Mpaka dakika 45′ za kipindi cha kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.
TAKWIMU ZA KIPINDI CHA KWANZA ZILIKUWA HIVI
Kipindi cha pili BDF walianza kwa kasi na kasawazisha goli.
Walionekana kuamka na kushambulia, lakini mabeki wa Yanga waliendelea kuonesha ukomavu wao.
Dakika ya 72′, Danny Mrwanda alitolewa nje kwa kadi nyekundu kufuatia kumpiga kiwiko mchezaji wa BDF. Kadi hiyo ilitoka kwasababu alipata kadi mbili za njano.
BDF waliendelea kulishambulia lango la Yanga na katika dakika ya 85′ Madziba Mosimanyana aliiandikia BDF bao la la pili baada ya mabeki wa Yanga kuzembea.
Mpaka dakika 90′ zinamalizika BDF 2 Yanga 1.


Comments