Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema kikosi chake kipo sawa kwa ajili ya mechi ya kesho dhidi ya Stand United, 'Chama la Wana'.
Simba itakuwa na kazi ya kuwania pointi tatu muhimu dhidi ya Stand ambayo imepania kushinda.
Kopunovic amesema kila kitu kinakwenda vizuri na anaamini watafanya kile wanachotaka kushinda.
"Tunaheshimu kuwa Stand ni timu ya ligi kuu, itakuwa inataka pointi tatu kama sisi. Hii inaonyesha itakuwa mechi ngumu.
"Kikubwa tunajua tunatakiwa kucheza kwa umakini mkubwa na kujituma, lengo ni kushinda na ninaamini itafanikiwa," alisema.
Simba ina siku tatu mjini Shinyanga ikisubiri kuwavaa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage.
Comments
Post a Comment