KOCHA mkuu wa Simba SC, Mserbia, Goran Kopunovic, jana hakuwa na mpango wa kuongea na waandishi wa habari baada kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage,Shinyanga.
Hata hivyo wanahabari 'mapaparazi' hawashindwi kitu, walimfuata na kumuweke vinasa sauti wakimtaka atie neno kwa ajili ya wasikilizaji, wasomaji na watazamaji.
Akiwa hana hamu ya kuongea, Kopunovic alisema : "Ligi ni ngumu, mechi ilikuwa kama fainali. Nimeona timu zinaikamia Simba, lakini bado tutaendelea kujiandaa kwa kila mechi iliyombele yetu".
"Tunafanya kazi kwa juhudi, kwa asilimia 100 niifundisha timu, matokeo yamekuwa ya kupanda na kushuka, kwa pamoja tutapata mafanikio"
Machi 8 mwaka huu, Kopunovic atawavaa Yanga katika mechi ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Huu utakuwa mtihani mkubwa kwa Mserbia huyo kwani mechi zinazowakutanisha watani wa jadi Tanzania (Simba na Yanga) huwa zinachangia kufukuzwa kwa makocha.
Comments
Post a Comment