Kikosi cha Yanga kinachoanza Botswana hiki hapa………….


DSC_0863-794466

KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameweka wazi kikosi chake kinachoanza leo katika mechi ya marudiano ya kombe la Shirikisho inayopigwa mjini Gaborone , Botswana dhidi ya wenyeji BDF XI kuanzia majira ya saa 12:00 jioni.

Mechi ya kwanza jijini Dar es salaam,  februari 14 mwaka huu, Yanga walishinda 2-0, mabao yote yalifungwa na Amissi Tambwe.

KIKOSI KIKO HIVI

Golikipa ni Ally Mustapha 'Bartezi, beki wa kulia ni Mbuyu Twite, kushoto Oscar Joshua.

Mabeki wa kati ni Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kelvin Patrick Yondan 'Cotton'.

Kiungo namba sita ni Said Juma, winga wa kulia ni Mrisho Ngasa. Tofauti na mawazo ya wengi, Saimon Msuva ameanza namba 8.

Mshambuliaji wa kati ni Amissi Tambwe, nyuma yake anacheza Danny Mrwanda na winga wa kushoto ni Haruna Niyonzima.

WACHEZAJI WA AKIBA: Deo Munishi 'Dida', Rajab Zahir, Jerryson Tegete, Salum Telela, Pato Ngonyani, Hussein Javu na Kpah Sherman.



Comments