Klabu ya Kagera Sugar leo inefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Morogoro katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara mchezo uliopigwa klatika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Bao hilo ambalo limeifanya Kagera Sugar kufikisha pointi 24, limefungwa na Rashid Mandawa katika dakika ya 38 baada ya kupiga shuti kali kwa mguu wa kushoto.
Hivi ndivyo ilivyo kuwa katika mchezo huo.
Kagera wanapata kona ya kwanza katika dakika ya 3 inayochongwa na Salum Kanoni lakini Kipa wa Polisi Morogoro anaunyaka na kuanza mashambulizi Upya.
Dakika ya 5 Kagera Sugar wanakosa bao baada ya kupata faulo ambayo inapigwa na Juma Mpola kwa shuti kali ambalo linagonga mwamba wa juu na kurudi ndani ambapo inamkuta Mshambuliaji wa Kagera ambaye pia anapiga Shuti ambalo linapaa juu.
Said Bahanuzi wa Polisi Moro anakosa bao katika dakika ya 9 baada ya kupewa pasi ya chini lakini anakumbana na vikwazo vya mabeki wa Kagera na kujikuta anapiga shuti ambalo linapaa nje ya lango la Kagera.
Dakika ya 15 Polisi Moro wanapata kona ya kwanza ambayo inachongwa bila mipango na kuangukia katika miguu ya mabeki wa Kagera na Kuosha mbele.
Rashid Mandawa katika dakika ya 17 anakosa bao la wazi baada ya kupenyezewa pasi ya chini akiwa yeye na Kipa lakini anapiga shuti kali ambalo linapaa juu na kuwaacha mashabiki wa Kagera wakibaki midomo wazi kwa mshangao.
Dakika ya 20 Salum Kanoni anapiga Free Kick baada ya Rashid Mandawa kufanyiwa madhambi na beki wa Polisi Moro lakini malengo yanakuwa hayatimii baada ya kupiga Fyongo.
Dakika ya 22 Said Bahanuzi anaiandikia Polisi Morogoro bao kufatia mpira wa kona lakini Mwamuzi wa mchezo huo Amon Paul anasema sio bao kwani alikuwa ameibia.
Mshambuliaji wa Kagera Sugar Atupele Green, anapiga Shuti zaidi ya mita 30 lakini linatoka nje ya lango la Polisi Morogoro hiyo ikiwa ni dakika ya 6 ya mchezo huo
Kagera wanapatra kona ya pili katika dakika ya 36 lakini inakuwa haina macho kwani mabeki wa Polisi Moro wanakuwa makini kuokoa mpira huo na kujipanga upya.
Dakika ya 38 Mshambuliaji wa Kagera Sugar, Rashid Mandawa anaipatia timu yake bao la kwanza kufatia shuti kali alilopiga kwa mguu wake wa kushoto na kumuacha kipa wa Polisi Moro Ibada Abdul akiwa hana cha kufanya.
Atupele Green wa Kagera anakosa bao baada ya kupiga mpira ambao unakuwa sio chochote sio lolote kwa kipa wa Polisi Moro.
Dakia ya 45 Polisi moro wanapata faulo karibia na 18 ya kagera Sugar lakini mpigaji anakuwa hayuko makini kwani vipimo vinazidi uwezo na mpira kupaa juu zaidi.
Hadi dakika ya 45 za kwanza zinamalizika na muamuzi Amon Paul kutoka Mara anapuliza kipenga cha mwisho Kagera Sugar wanaongoza kwa bao 1-0 ambalo limefungwa na Rashid Mandawa huku wakiongoza kwa kupiga mashuti mara 3 ambayo yote yalilinga lango, huku Polisi Moro wakipiiga mashuti 2 tu ambayo hayakulenga lango.
Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi Polisi Moro wanaanza kwa kushambulia kwa kasi lango la Kagera na kufanikiwa kupata bao kunako dakika ya 46 lakini Mwamuzi kwa mara ya pili anakataa bao akisema ni offside yaani kaibia, kitu ambacho kinafanya wachezaji wa Polisi Morogoro wamfate mshika kibendera na kumzonga kiashirio hawakukubari na uamuzi huo.
Dakika ya 51 polisi wanafanya mabadiriko anatoka Salum Kihimba na kuingia Imani Mapunda.
Kagera sugar wanakosa bao baada ya Atupele Green ambapo anapiga mpira unaopaa juu ikiwa ni dakia ya 53.
Dakika 58 Bahanuzi anaikosea bao la wazi Polisi Moro baada ya kuwepo na penyeza nzuri ya wachezaji wa maafande hao na kumuacha kipa wa Kagera lakini umaliziaji wa kazi ukawa duni.
Dakika ya 60 Kagera wanafanya mabadiriko anaingia Babu Ally na Juma Mpora anakwenda benchi.
Polisi Morogoro wanapata kona kunako dakika ya 69 inayopigwa na Hassan Mganga lakini inakuwa haina macho kwa kipa wa Kagera Agaton Antony.
Kagera Sugar wanafanya mabadiriko mengine na kumtoa Adam Kingwande ambaye nafasi yake inachukuliw na Paul Ngwai ikiwa ni dakika ya 72.
Dakika ya 79 Kagera Sugar Sugar wanakosa bao baada ya Rashid Mndawa kupiga Shuti ambalo linaangukia kwa kipa wa Polisi Moro.
Dakika ya 80 ya mchezo huo Bahanuzi anakosa bao baada ya kubakia na kipa wa Kagera Sugar na kuambulia kutoa mpira nje.
Hadi dakika ya 90 zinamalizika Muamuzi Amon Paul kutoka Mara, anapuliza kipenga cha mwisho, Kagera sugar walikuwa wakiongoza kwa bao 1-0 ambalo limefungwa katika kipindi cha kwanza.
Comments
Post a Comment