Juventus Italia imeanza vizuri kampeni zake za kusaka tiketi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kufuatia ushindi mwembamba wa 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tevez aliwapa wenyeji bao la kwanza kunako dakika ya 18 kabla ya Marco Reus kuchomoa dakika ya 18. Dakika ya 43 Juventus wakafunga bao lao la pili kupitia kwa Morata.
Hata hivyo Borussia Dortmund inajipa matumaini na faida ya bao lao la ugenini na hivyo kuhitaji ushindi wa bao 1-0 nyumbani ili kusonga mbele.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo (Pereyra 37), Pogba, Vidal (Padoin 86), Tevez (Coman 89), Morata.
Borussia Dortmund: Weidenfeller, Piszczek (Ginter 32), Papastathopoulos (Kirch 46), Hummels, Schmelzer, Gundogan, Sahin, Aubameyang, Mkhitaryan, Reus, Immobile (Blaszczykowski 75).
Comments
Post a Comment