JOSE MOURINHO AICHAMBUA ARSENAL …ASHANGAA KWANINI IPO HAPO ILIPO


JOSE MOURINHO AICHAMBUA ARSENAL …ASHANGAA KWANINI IPO HAPO ILIPO

Mourinho was speaking on Sky Sports' Goals on Sunday              after Chelsea's controversial draw with Burnley

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema haelewi ni kwanini Arsenal ipo hapo ilipo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Akizungumza na Sky Sports siku ya Jumapili, Mourinho alidai kuwa kwa ubora wa timu iliyo nayo Arsenal, umahiri wa wachezaji na aina ya soka lao, timu hiyo ilistahili kuwa juu ikipigania taji.

Arsenal iko katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, lakini imetenganishwa na pointi 12 kati yake na vinara Chelsea. Timu hizo zitapambana April 26 kwenye dimba la Emirates ikiwa ni miongoni mwa mechi za ukingoni ukingoni mwa Ligi Kuu.

"Arsenal ina wigo mkubwa wa washambuliaji - [Alex] Oxlade-Chamberlain, [Mesut] Ozil, [Theo] Walcott, [Santi] Cazorla, [Tomas] Rosicky, Alexis [Sanchez] – ni kikosi cha ajabu.

The Chelsea boss says he likes Arsenal's team 'very              much', noting attacking options such as Alexis Sanchez

"Napenda namna namna wanavyocheza na nafikiri ni timu nzuri," alisema Mourinho.

Arsenal wamekwenda miaka tisa bila taji kubwa chini ya Arsene Wenger na ingawa ukame huo ulikatika msimu uliopita baada ya kutwaa taji la FA, Mourinho anasisitiza alitegemea upinzani mkubwa kwa Arsenal msimu katika mbio za Ligi Kuu.

"Arsenal? Sielewi kwanini hawako pamoja nasi na Manchester City kileleni," alisema Mourinho.

"Naipenda sana timu yao, ina wachezaji wazuri, Alexis [Sanchez] na [Danny] Welbeck wameongeza ubora ndani ya kikosi bora walichokua nacho.

"Katika kipindi hiki Wenger yupo na kazi ambayo sote tungependa kuwa nayo. Kila meneja duniani anapenda kuwa na uimara alionao mwaka hadi mwaka huku akiwa na nafasi ya kununua, kuuza na kujenga timu, kusubiri mafanikio… kusubiri na kusubiri. Nadhani ana kazi ambayo ni njozi za kila mmoja."



Comments