JICHO LANGU LA TATU; ‘ Ni lazima Aveva aombe radhi kuinusuru Simba SC’


JICHO LANGU LA TATU; ' Ni lazima Aveva aombe radhi kuinusuru Simba SC'

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Ni wakati mwafaka kwa rais wa Simba SC kukubali makosa yake. Kwanza muda unakwenda kasi sana, Pili ni rekodi mbaya ya timu katika ligi kuu, Tatu wale wapinzani wake wamekuwa na nguvu kubwa. Kusema kweli, tangu ameingia madarakani katikati ya mwaka uliopita ( Juni, 2014), Aveva amekuwa katika presha kubwa kiasi cha kumfanya azunguke na timu hiyo ' huku na huko' kama njia ya kuwaongezea hamasa na hali wachezaji wake.

evans
Simba ilikutana na kipigo cha nne msimu huu mbele ya Stand United siku ya Jumapili katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga na kuporomoka hadi katika nafasi ya saba ya msimamo. Kila 'mtu wa Simba' yuko katika presha, licha ya kuwa na wachezaji wenye uwezo timu hiyo imefanikiwa kushinda mara nne tu katika michezo 15 waliyokwishacheza msimu huu, wakiwa na rundo la sare ( sare 8), timu hiyo tayari imepoteza pointi 25.
Kufungwa bao 1-0 na Stand United inamaanisha kuwa Simba imefanya ngazi na timu hiyo ambayo sasa mefiksha alama 21 ' moja zaidi ya Simba'. Simba mefunga magoli 14 na kuruhusu 11, inaonesha wazi kuwa timu hiyo ni dhaifu katika idara nyingi ndani ya uwanja lakini n hivyo pia hadi katka utawala na huko ndiko ' kiini' cha kuvurunda kwa tmu hiyo kilipo. Inawezekana timu hiyo ikawa inahitaji muda na vipaji zaidi ili kunyanyuka, ila ni lazma matatizo ya umoja yatatuliwe na kurudishwa klabuni hapo.

Aveva aliwavutia baadhi ya wanachama kwa sera yake ya ' vidole3′ wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, Juni, 2014 lakini sera hiyo imekuwa tatizo kubwa ndani ya miezi kumi sasa tangu alipoingia madarakani kwa wingi wa kura. Utaratibu alioutumia katika mkutano wake wa kwanza kama rais wa klabu naamini haukuwa mzuri.

Mengi yanazungumzwa na yataendelea kuzungumzwa kuhusu hatma ya Simba msimu huu kwa kuwa wengi walitaraji uongozi mpya ungekuja na mikakati mipya ya kurudisha makali ya Simba ambayo tayari yalipotezwa na utawala wa Mh. Aden Rage. Baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu msimu wa 2012/13, kisha kushuka hadi nafasi ya nne msimu uliopita, Simba iko nyuma ya vinara Yanga SC kwa tofauti ya pointi 11, ni gemu kubwa kwa timu kama Simba.
Sifikiri kama Aveva alifanya vizuri kuwafuta uanachama wa klabu zaidi ya watu 72, alijikuza na kujipa heshima kubwa akimaanisha hakuna aliye juu yake. Ndiyo, wale wanachama walikuwa karibu kuvunja kanuni za soka kwa kupeleka mambo ya soka katika mahakama za kawaida, ila wakati mwingine mahakama ni sehemu ambayo haki na usawa vinaweza kupatikana. Unaweza kuwasikiliza baadhi ya watu wakisema kuwa Simba haitatetereka licha ya kuwepo kwa ' Simba Ukawa' lakini upande wangu naamini tofauti.

Nachukulia uamuzi wa kuomba radhi na kuwarudishia uanachama ' wanachama waliofutwa' ndiyo njia sahihi ya Aveva kufanikisha malengo yake ya kuiongoza Simba. Naweza kusema hadharani kuwa Simba itaendelea kutetereka kama rais wa klabu hiyo ataendelea kujiweka juu na kukubali 'nguvu ya ushawishi' waliyonayo ' Simba Ukawa' ambayo inaendelea kusambaa na kukomaa kutokana na matokeo mabaya.
Aveva hakuwa chaguo la wote, lakini namna mchakato wa uchaguzi ulivyoendeshwa wanachama walilazimika kumchamgua. Simba ilihitaji 'mtu hasa wa utawala', ilihitaji mtu hasa wa utawala ambaye angeweza kurudisha umoja uliopotea tangu Juni, 2012 ndiyo maana majina kama ya Andrew Tupa, Michael Wambura yalijitokeza kuwania nafasi ya juu zaidi sambamba na Aveva. Chaguo la Aveva lilikuwa sahihi lakini wengi walisahau kuwa nyuma yake watafuata watu 'wajanja, wajanja' na kutengeneza timu ya utawala.

Hakuna maelewano katika utawala hadi sasa, uku wakinyosheana vidole vya lawama ni wazi rais huyo wa klabu ' hana meno' huku wenzake wakitumia udhaifu wake huo ' kumkontroo kwa rimoti'. Wachezaji wamekuwa wakicheza kwa kujituma lakini mwisho wa siku matokeo yanakuja ya kusikitisha. Wachezaji wengi wamekuwa wakipambana ndani ya uwanja lakini kwa kutambua hilo, utawala unapaswa kutafuta chanzo cha kufanya vibaya.
Kwa kuwa mpira unaongozwa na watu wa mpira na wenye uchumi mzuri, unaweza kuamini kuwa Simba itafanya vizuri chini ya utawala wa Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange Kaburu. Huwezi kuacha kuwapongeza Aveva na Kaburu kuhusu mazuri waliyoifanyia Simba, lakini katika utawala unaohitaji nguvu kubwa ya ujamaa viongozi hao wamekosa mipango mizuri. Wamekuwa ni watu wa kutafuta 'mtu wa kafara',
Amri Kiemba, Haroun Chanongo, Patrick Phiri na Shaaban Kisiga wameondolewa kwa sababu za kufikirika na sababu za kutengenezwa, kulikuwa na sababu za wanne hao kuondolewa?
Ni wakati sahih sasa kwa Aveva kuomba radhi wanachama aliowatimua ili kurudisha umoja wa kweli Simba SC, vinginevyo wataendelea kuchapwa msimu huu….

0714 08 43 08



Comments