JICHO LANGU LA TATU; ‘ Baada ya kuchapwa 3-1 na Monaco, Arsenal inahitaji majina makubwa zaidi na si…..’


JICHO LANGU LA TATU; ' Baada ya kuchapwa 3-1 na Monaco, Arsenal inahitaji majina makubwa zaidi na si…..'

2617E59F00000578-0-image-a-7_1424897669721

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam, 

Maana halisi ya ' ligi ya mabingwa ulaya' huwa na uzito mkubwa wakati klabu nane zinapokuwa zikisubiri upangwaji wa ratiba ya robo fainali. Itakuwa ni maajabu kwa klabu iliyocheza michuano 17 kushindwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali kwa misimu mitano mfululizo huku ikiwa na matumizi makubwa ya pesa. Arrenal wapo karibu kupoteza ' mvuto' katika michuano ya mabingwa ulaya endapo itashindwa kufuzu kwa robo fainali kwa misimu mitano mfululizo.

 

 

Ikicheza katika uwanja wa nyumbani, Emirates katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 dhidi ya AS Monaco timu hiyo ya London ' ilinyanyaswa' kisha kufungwa ' kifungo cha kufadhaisha' cha magoli 3-1. Arsenal chini ya mkufunzi, Arsene Wenger ilifuzu robo fainali ya mabingwa kwa mara ya mwisho msimu wa 2009/10 na kuondolewa na FC Barcelona, baada ya hapo mafanikio makubwa ya timu hiyo ni kujaribu ' kukomboa rundo ya magoli' katika michezo ya pili ya hatua ya 16.

 

 

Wenger alikuwa na ' usiku mbaya zaidi' katika michuano hiyo baada kukubali kipigo kikubwa cha kwanza katika uwanja wa nyumbani. Lakini tangu walipopambana kusawazisha na kutengeneza ushindi mabao 2-1 dhidi ya Barcelona katika uwanja wa Emirates, Februari, 2011, Arsenal haijawahi kuwa tishio katika michuano hiyo.

 

 

Walichapwa 4-0 na AC Milan katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 katika uwanja wa San Siro kabla ya kuwashinda Wataliano hao kwa mabao 3-0 katika mchezo wa marejeano pale Emirates. Licha ya ushindi huo mkubwa, Arsene alishuhudia kikosi chake kikishindwa kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya pili mfululizo. Msimu miwili iliyopita mara zote wamekwama mbele ya Bayern Munich.

 

Safu ya ulinzi ilikuwa dhaifu mno na hata kiongozi Per Mertesacker alishindwa mara kadhaa kujipanga katika nafasi. Wakati Anthony Marial anampasia pasi ya mwisho Berbatov aliyekuwa ndani ya eneo la hatari upande wa kulia, Mertesacker na patna wake Laurent Koscielny hawakuwa katika maeneo sahihi na mfungaji akafunga bao ambalo liliwafanya Arsenal kuwa nyuma kwa mabao 2-0 kufikia dakika ya 53.

 

Goli la tatu lilimfadhaisha kila mtu wa Arsenal kwa kuwa waliamini kuwa kitendo cha Alex Oxlade-Chamberlain kuifungia timu yake bao la kufutia machozi katika dakika ya 90+1 ni sawa na kurudisha matumaini yao ya kufika walau robo fainali msimu huu, lakini umakini mdogo  katika kujilnda ulisababisha wakachapwa bao katika dakika ya mwisho kabisa 90+5 na Yannick  Ferreira ambaye alimalizia mpira wa Bernardo Silva.

 

Itakuwa ni ' miujiza' kuona Arsenal ikiwa miongoni mwa klabu nane ambazo zitafuzu kwa robo fainali ila itashangaza zaidi endapo timu hiyo itaondolewa na Monaco, timu ambayo inacheza Ligue 1 kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kupada kutoka Ligue 2 miaka miwili iliyopita. Wenger anahitaji wachezaji wa namna gani sasa ili Arsenal ipae?.

 

 Kwanza ni kufanya usajili wa majina makubwa mawili hadi matatu msimu ujao ili kuleta uzito katika timu. Barcelona walitumia usajili wa pesa nyingi ili kurejea katika michuano ya ulaya, Milan, Real Madrid na sasa Manchester United zote hizo ni klabu ambazo zinanunua wachezaji wenye majina makubwa kwa lengo la kufanikiwa kupitia wao.

 

Si tu kununua wachezaji wa gharama, hapana, Wenger anahitaji kuijenga Arsenal katika mfumo wa ' kuogopwa' na majina makubwa katika timu husaidia kuwaonya wapinzani. Mesut Ozil, Sanchez, Welbeck hawa ni wachezaji wenye gharama kubwa lakini Je ni wachezaji sahihi ambao timu inapaswa kuwatumia kama ' kinga' dhidi ya wapinzani wao?. Wenger asilaumiwe kwa kipigo hiko, wachezaji wamefanya uzembe mkubwa.

0714 08 43 08



Comments