JAHAZI MODERN TAARAB ‘KUITEKA’ BUGURUNI IJUMAA HII …Mahaba Niue ya Mzee Yussuf yasubiriwa kwa hamu



JAHAZI MODERN TAARAB 'KUITEKA' BUGURUNI IJUMAA HII …Mahaba Niue ya Mzee Yussuf yasubiriwa kwa hamu
JAHAZI MODERN TAARAB 'KUITEKA' BUGURUNI IJUMAA HII            …Mahaba Niue ya Mzee Yussuf yasubiriwa kwa hamu

Ijumaa hii pale Lekam Royal Pub maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, kutakuwa na burudani kubwa ya muziki wa mwambao kutoka kwa Jahazi Modern Taarab.

Lekam Royal Pub ni kiwanja kipya cha burudani chenye ukubwa wa aina yake na madhari ya kipekee pamoja na usalama wa hali ya juu huku kukiwa na eneo la kumwaga la maegesho (parking) ya magari.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Jahazi kupiga hapo tangu ukumbi huo ufunguliwe na hivyo kulifanya onyesho hilo liwe gumzo huku Mzee Yussuf akisubiriwa kwa hamu kubwa na wimbo wake mpya wa "Mahaba Niue".

Mratibu wa onyesho hilo, Juma Mbizo ameiambia Saluti5 kuwa maandalizi yote ya burudani hiyo yamekamilika na kinachosubiriwa sasa ni wasaa tu wa Jahazi kufanya kile kinachotarajiwa.



Comments