Ilikuwa hivi Azam FC ikibanwa mbavu na Ruvu Shooting



Ilikuwa hivi Azam FC ikibanwa mbavu na Ruvu Shooting

azamNa. Richard Bakana, Dar Es Salaam

MABINGWA watetezi wa Ligi kuu ya Tanzanaia bara na wawakirishi wa klabu Bingwa, Azam FC leo wamejikuta wakigawana pointi tatu na wenyeji wao Ruvu Shooting katika mchezo ambao umepigwa kunako uwanja wa Mabatini Mlandizi Mkoani Pwani.

Dakika ya 6 Azam walipata kona iliyopigwa na Himid Mao Mkami lakini inakuwa sio chochote kwani inageuka kuwa mboga ya kipa wa Ruvu shooting.

Kunako dakika ya 9 Azam wanapata Faulo baada ya Mdathiri Yahya kufanyiwa madhambi lakini Kipre Tchtche anapiga mpira ambao unatoka nje kabisa ya lango la Ruvu.

Ruvu wanapata faulo baada ya Michael Idan kufanyiwa madhambi na Erasto Nyoni lakini mchezaji huyo huyo anapiga mpira ambao hauna madhara kwa Azam ikiwa ni dakika ya 15.

Dakika ya 19 Salum Abubakar Sure boy anapiga krosi ambayo inamkuta John Bocoo katika 18 ya Ruvu lakini kwa kuzongwa na mabeki wa Wanajeshi hao Bocco anaunawa mpira huo na kuwekwa chini.

Ilikuwa ni dakika ya 21 Azam wanapata kona ya pili ambayo inachongwa na Erasto Nyoni lakini inakuwa haina Marengo baada ya kuangukia miguuni mwa beki wa Ruvu Shooting.

Dakika ya 24 Kipre Herman Tchetche anapata nafasi ya wazi ya kufunga bao lakini anapiga shuti kali ambalo linatoka nje baada ya kukatika kwa Upepo.

Dakika ya 34 Azam wanakosa bao baada ya Kipre Tchetche kupiga krosi safi ambayo inamkuta John Bocco lakini inamgonga katika paja la mguu wa kulia na kutoka nje.

Kunako dakika ya 35 Pascal Wawa anakosea baada ya mpira kumponyoka miguuni na kuangukia kwa Michael Idan ambaye anapiga shuti lakini kipa Aishi Manula anakuwa makini kuudaka na kuokoa bao hilo.

Dakika ya 42 Ruvu wanapata kona ya Kwanza ambayo inachongwa na Amis Kasanga  lakini inakosa macho baada kuokolewa na mabeki wa Azam FC.

Dakika ya 45 Shomali Kapombe anapiga krosi ambayo haizai chochote kwani inatoka nche na kufanya vijana wa Ruvu Shooting kujipanga upya kuendelea kusaka bao la kuongoza.

Hadi Mwamuzi wa mchezo huo Livingstone anapuliza kipyenga kuashiria dakika 45 za kwanza zimemalizika, timu zote zilikuwa hazijafungana huku Ruvu wakionekana kumiliki mpira kwa asilimia 52 na Azam FC kwa asilimia 48.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo katika dakika ya 64 Michael Idan alifanyiwa madhambi na Erasto Nyoni Nje kidogo ya 18 ya lango laAzam FC lakini mpira huo wa adhabu haukuweza kuleta madhara kwa Wanalamba lamba hao au Baraka kwa wanajeshi hao.      

Dakika ya 67 Ruvu Shooting wanafanya mabadiliko, ambapo Kocha Thom Olaba anaamua kumpumzisha Hamis Saleh na nafasi yake anaingia Charles Chagula.

 Dakika 79 Baraka Mtuwi wa Ruvu Shooting anaingia kuchukua nafasi ya Juma Hade.

John Bocco anakosa bao kunako dakika ya 80 baada ya kupiga shuti kali lakini mlinda mlango  Rashid Abdullah kipa Ruvu Shooting anaupangua.

Dakika ya 82 Aishi Manula anaokoa free kick ambayo ilipigwa kwa shuti kali na Michael Idan kufata madhambi ambayo alifanyiwa na mabeki wa Azam FC.

Baraka Mtuiwi anapewa kadi ya njano na muamuzi Livingstone baada ya kumfanyia madhambi Mudathiri kunako dakika ya 85.

Kocha Joseph Omog anaamua kumpuzisha Kipre Tchetche kunako dakika ya 88 na nafasi yake anaingia Kelvin Friday.

Hadi kipindi cha mwisho yaani dakika 90 zinamalizika mwamuzi Livistone anapuliza kipenga cha mwisho timu zote zilikuwa hazijaona lango la mwenzake licha ya Azam FC kufanikiwa kupiga mashuti 7 yaliyolenga lango na wenyeji wao Ruvu Shooting wakipiga mara 6.

Kwa upande wa mashuti yaliyotoka pembeni mwa lango Azam FC walipiga mara 4 sambamba na wapinzani wao ambao pia alipiga mara 4, Azam walipiga kona 2 huku wanajeshi hao wakipiga kona 3.

Katika mchezo huo Azam FC walionekana kucheza madhambi mengi baad ya kufanya madhambi mara 20 huku wanajeshi hao wakifanya madhambi mara 13 tu lakini wakizidiwa kumiliki mpira kwa Azam asilimia 52 na Ruvu asilimia 48.



Comments