Tangu aanze kuchezeshwa kama kiungo mkabaji, Wayne Rooney akajikuta anaingia kwenye ukame wa magoli ambapo amecheza dakika 952 bila kutupia mpira wavuni.
Nahodha huyo wa Manchester United hatimaye jana usiku akamaliza ukame huo kwa kufunga bao la penalti kunako dakika ya 88 katika mchezo wa FA dhidi ya Preston.
Bila kujali utata wa penalti yenyewe ilivyokuja ambapo ilionekana wazi kuwa Rooney kamdanganya mwamuzi, lakini mchezaji huyo ambaye pia ni nahodha wa England, akatuliza akili na kumchambua kipa Thorsten Stuckmann.
Kocha Van Gaal ameendelea kusisitiza kuwa ataendelea kumtumia Rooney kama kiungo licha ya kelele nyingi kutoka kwa wachambuzi wa soka Uingereza.
Comments
Post a Comment