Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzanaia, Taifa Stars, pamoja na klabu ya Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amesema kuwa bado analidai shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF pesa zake za posho alipokuwa akiitumikia timu hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa kupitia runinga ya East Africa, Maxime ambaye kwa sasa ni Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, amesema kuwa deni hilo limekuja baada ya kupigwa danadana sana zilipokuwa zinatokea safari au timu inatakiwa iingie kambi kwa maandalizi ya mchezo.
"Wachezaji wa tiu ya Taifa siku hizi wanaraha, timu inawadhamani, nakumbuka tumewahi kwenda Zambia kwa basi, Mimi hadi leo bado nadai hela zangu lakini ndio hivyo tena tulikuwa tunatumikia Taifa" Amesema Maxime, lakini sio kwamba yupo kwenye mchaka wa kuzidai.
Maxime amesema kuwa walikuwa wakilimbikiziwa madeni kitu ambacho kimefanya asamehe, "Sasa utaenda wapi kudai"
Maxime alikuwa akiiongoza Taifa Stars kama nahodha enzi za Uongozi wa kocha Mbrazil Marcio Maximo.
Comments
Post a Comment