George Kavila ; ‘ Kila kitu kinakwenda sawa Kagera Sugar…’


George Kavila ; ' Kila kitu kinakwenda sawa Kagera Sugar…'

DSC_0996

George Kavila (kushoto) akikabiliana na Elias Maguli desemba 26 mwaka jana Simba wakichapwa 1-0.

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,

Malengo makubwa ya Kagera Sugar msimu huu ni kuwa miongoni mwa klabu tatu ambazo zitamaliza ndani ya nafasi tatu za juu. Kagera ambayo kwa sasa wanautumia uwanja wa Kambarage, Shinyanga kama uwanja wao wa nyumbani kufuati uwanja wa Kaitaba kuwa katika matengenezo makubwa. Ikiwa katika nafasi ya tatu katika msimamo timu hiyo ya Bukoba itacheza na ' wenyeji halisi wa Kambarage Stadium' Stand United katika mchezo wa ligi kuu Bara kesho Jumamosi.

 Mchezo huo unaraji kuwa mkali kwa kuwa Stand imejiimarisha na kushinda michezo kadhaa ukiwemo ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC wiki iliyopita. " Kila kitu kinakwenda vizuri, tuna hali ya kupambana. Tayari tumecheza michezo migumu msimu huu na pengine gemu dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Ruvu ndizo zilikuwa ngumu zaidi upande wetu msimu huu lakini kiujumla ligi ni ngumu na hatujachoka kupambana" anasema George Kavila mchezaji wa Kagera Sugar kwa msimu wa tano sasa.

 Kagera imekuwa na kawaida ya kuanza msimu vizuri lakini humaliza ligi vibaya kiasi cha kufanya imalize katika nafasi za nne msimu wa 2012/13 na nafasi ya tano msimu wa 2013/14 licha ya kuwa na matokeo mazuri katika michezo ya mwanzo. Uzoefu mdogo umekuwa ukitajwa kama sababu ya kufanya vibaya kwa timu hiyo mwishoni mwa msimu na hivyo hushindwa kutimiza malengo yake.

 " Tubataka kuendelea kucheza mechi zetu na kupata matokeo mazuri mazuri, hatutaki kuangalia timu nyingine zinafanya nini ama timu gani inacheza na nani. Tutazidi kuwa bora msimu huu mpaka siku ya mwisho na kutimiza malengo yetu ya kuingia 'top3'. Siku zote tunapambana huku tukizipa heshima kubwa klabu pinzani, hakuna timu ambayo tunaiogopa" anasema mchezaji huyo ambaye kwa mara ya kwanza alicheza ligi kuu Tanzania Bara mwaka 1998 aliposajiliwa na Coastal Union ya TaNGA. Kavila amewahi kuzichezea klabu za Coastal, 1998-2004, Twiga Sport, 2004-05, Polisi Moro, 2006, Moro United na tangu mwa ka 2009 amekuwa katika klabu ya Kagera Sugar.



Comments