Diego Costa amerejea dimbani wakati Chelsea ikitoa sare ya 1-1 kwa Paris Saint-German baada ya kuwa nje kwa adhabu ya wiki tatu.
Costa hakuwa kwenye kiwango chake kama Mourinho alivyobashiri, lakini bado akawa tishio kwa mchezo wake wa kibabe uliojaa nguvu nyingi.
Uwepo wake uliwaondolea utulivu mabeki wa PSG aliokuwa akiwasukuma huku na kule, akashinda mipira mingi ya kurusha na kona na muda wote akaonekana ni mtu wa kuleta misukosuko kwa wachezaji wa upinzani.
Comments
Post a Comment