CRISTIANO RONALDO, CASILLAS, CARLO ANCELOTTI WAANDIKA REKODI MPYA KWA USHINDI …Real Madrid yaicha Barcelona kwa pointi 4 safi



CRISTIANO RONALDO, CASILLAS, CARLO ANCELOTTI WAANDIKA REKODI MPYA KWA USHINDI …Real Madrid yaicha Barcelona kwa pointi 4 safi

The forward duo celebrate after the France striker              (left) scored the opening goal for Real against Elche on              Sunday night

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa tatu kwa kuifungia Real Madrid magoli mengi zaidi baada ya kufikisha mabao 290  wakati klabu yake ikiichapa Elche 2-0 katika mchezo wa La Liga Jumapili usiku.

Ushindi huo umeikita Real Madrid kileleni kwa pointi nne safi mbele ya Barcelona ambayo iliteleza Jumamosi kwa kukubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Malaga.

Kwa kutupia wavuni magoli 290, Ronaldo analingana na Santillana huku Alfredo Di Stefano akishika nafasi ya pili kwa kufunga magoli 305 wakati Raul anaongoza kwa magoli 323.

Cristiano Ronaldo clenches his fist in celebration              after scoring Real Madrid's second goal of the night against              Elche

Wakati Santillana alifunga magoli 290 katika mechi 645, imemchukua Ronaldo mechi mechi 281 tu kufikisha idadi hiyo.

Goli lingine la Real Madrid lilifungwa na Karim Benzima wakati kocha Carlo Ancelotti akifikisha kwa ushindi mchezo wake wa 100 wa kuikochi timu hiyo.

Carlo Ancelotti took charge of his 100th competitive              match of Real Madrid in the 2-0 win against Elche

Kipa Iker Casillas naye alikuwa na cha kujivunia katika mchezo huo baada ya kumaliza mchezo wake wa 500 kwa Real Madrid kwa ushindi muhimu huku lango lake likiwa halijaguswa.

Iker Casillas applauds the travelling supporters on              what was his 500th La Liga appearance for Real Madrid on              Sunday night

Elche (4-4-1-1): Tyton; Suarez, Roco, Lomban, Edu Albacar; Rodriguez, Adrian ( Herrera 81), Pasalic (Galvez 75), Niguez (Mendes Rodrigues 64) ; Fajr; Jonathas.

Real Madrid (4-3-3): Casillas; Carvajal, Pepe, Varane, Marcelo; Lucas Silva (Illarramendi 84), Kroos, Isco (Arbeloa 89); Bale, Benzema (Jese 93), Ronaldo.



Comments