Na Augustino Mabalwe
Kuelekea mchezo wa fainali wa kombe Capital- one kati ya Chelsea na Tottenham Hotspurs utakopigwa jumapili hii katika uwanja wa Wembley,kipa wa klabu ya Chelsea Thibaut Courtois amesema anazijua mbinu za kumzuia mshambuliaji wa wapinzani wao Harry Kane.
Kane ambaye ni zao la Spurs, amekuwa katika kiwango kizuri na mpaka sasa ameshafunga magoli 24 katika mechi zote alizocheza katika michuano mbalimbali msimu huu.
Hivyo mchezo huu wa jumapili ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa hizo ni nafasi nyingine kwa Kane kudhihirisha ubora wake.
Licha ya Kane kushinda magoli mawili katika mechi ambayo Tottenham Hotspurs iliibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa ligi kuu Januari mosi mwaka huu,lakini Courtois anaamini ataweza kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 katika mechi hiyo kali.
Chelsea imetinga hatua ya fainali baada ya kuitoa Liverpool katika hatua ya nusu fainali kwa jumla ya goli 2 kwa 1 huku Spurs ikiingia fainali kwa kuwatoa Sheffield United kwa jumla ya goli 3 kwa 2.
Fainali hii inajirudia ile ya mwaka 2008 ambayo Tottenham Hotspurs ilichukua ubingwa wa kombe hilo baada ya kuifumua Chelsea goli 2 kwa 1 katika mchezo huo.
Comments
Post a Comment