Vinara wa ligi kuu Chelsea, wakicheza kwao Stamford Bridge, wametoka Sare 1-1 na Burnley ambayo inapigana isishushwe daraja.
Chelsea walitangulia kufunga kwa bao la Branislav Ivanovic la dakika ya 14 lakini wakawa pungufu katika dakika ya 70 pale Nemanja Matic alipopewa kadi nyekundu alipolipizia rafu toka kwa Ashley Barnes. Burnley walisawazisha kwa bao la kichwa la Ben Mee kufuatia kona ya dakika ya 81.
Arsenal wakiwa ugenini walipata ushindi wa bao 2-1 walipoichapa Crystal Palace na kutwaa nafasi ya 3 kwa kuishusha Man United nafasi ya 4 mabao yakifugwa na Santi Carzola kwa mkwaju wa penati na Giroud.
Bao pekee la Palace lilifungwa dakika ya 90 na Glenn Murray.
Manchester City imepunguza pengo kwa Chelsea hadi kufikia pointi tano baada ya kuifumua Newcastle 5-0 kwa magoli ya Sergio Aguero, Samir Nasri , Edin Dzeko na David Silva aliyefunga magoli mawili.
Matokeo ya mechi zote zilizochezwa Jumapili ni:
Aston Villa 1 - 2 Stoke City
Chelsea 1 - 1 Burnley
Crystal Palace 1 - 2 Arsenal
Hull City 2 - 1 Queens Park Rangers
Sunderland 0 - 0 West Bromwich Albion
Swansea City 2 - 1 Manchester United
Manchester City 5 - 0 Newcastle United
Comments
Post a Comment