Na Augustino Mabalwe
Klabu ya Chelsea imetangaza kusaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya Yokohama Rubber wakiwa ndiyo wadhamini wapya wa matangazo ya jezi.
Mkataba huo wenye thamani ya paundi milioni 40 kwa mwaka unaifanya Chelsea kuwa klabu ya pili katika matangazo ya jezi katika vilabu vya Uingereza huku Manchester United wakishika namba moja kwa kuingiza paundi milioni 53 kwa mwaka kutokana na mkataba wao wa miaka saba na kampuni ya magari ya Chevrolet .
Chelsea imekuwa ikidhaminiwa na kampuni ya Samsung tangu mwaka 2006 ambao walikuwa wanaiingizia klabu hiyo paundi milioni 18 kwa mwaka.
Kampuni hiyo kutoka Tokyo nchini Japan ambayo inashughulika na utengenezaji wa matairi,vifaa vya majini na ujenzi wa viwanda pia inadhamini vilabu mbambali vinavyoshiriki ligi kuu ya kikapu nchini Marekani Nba kama vile Bolton,Celtic na San Antonio Spurs.
"Karibuni sana wadhamini wetu wapya Yokohama,ninaamini mahusiano yetu yatakuwa na faida sana na tutafika mbali zaidi " alisema mwenyekiti wa klabu ya Chelsea Bruce Buck.
Hivyo Chelsea ambao wapo kileleni katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza wataanza kuvaa jezi zilizoandika Yokohama rubber kuanzia msimu wa 2015/2016.
Comments
Post a Comment