Cannavaro avunja ukimya, awachambua Pluijm na Maximo



Cannavaro avunja ukimya, awachambua Pluijm na Maximo

Marcio-Maximo-1Na. Richard Bakana, Dar es salaam

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzanaia, Taifa Stars, pamoja na klabu ya Dar es salaam Young Africans, Nadir Haroub 'Cannavaro' amefunguka ya moyoni kwa kuzungumzia tofauti zilizopo kati ya makocha wake Marcio Maximo wa zamani na wasasa Hans Ven De Pluijm na kusema kuwa Mholanzi ni sheeedah.

Akizungumza na Shaffihdauda.com leo Asubuhi wakijiandaa kurejea Dar es salaam, Cannavaro amesema kuwa Maximo ni mzuri sana akiwa na timu za Taifa, lakini Pluijm anauwezo wa kumbadirisha mchezaji akawa katika hatua nyingine ya mafanikio.

Cannavaro amesema kuwa Maximo ambaye ndie aliemuibua na kumfanya aonekane enzi anakinoa kikosi cha timu ya Taifa, alipata shida sana akiwa na Yanga.

"Walimu wakotofauti hawa, ila tu kila mmoja anauzuri wake, Kwa mfano Maximo ,ndio kocha aliyenitoa chini hadi nikaja kuonekana, ni kocha ambaye ninamuheshimu sana, na kila kocha anamfumo wake,  Nadhani alipokuwa timu ya Taifa wachezaji wanatoka kwenye vilabu wakiwa moto kwahiyo ni kazi ndogo tu ya kuwaweka sawa tofauti na mwalimu akiwa kwenye klabu, Nadhani alipokuwa kwenye klabu yetu ndio alipata sana tabu" Amesema Cannavaro ambaye jana ameiongoza timu yake kujichimbia kunako kilele cha VPL kwa pointi 31 baada ya kuwafunga Mbeya City 3-1.hans pluijm

Kwa upande wa Kocha kutoka Uholanzi Hans Van De Pluijm, ambaye aliwahi kuinoa Yanga msimu uliopita kwa nusu msimu na kuiacha ikiwa katika nafasi ya pili ambapo alipata dili la kufundisha soka la Saudi Arabia, Cannavaro amesema anakiwango cha hari ya juu katika ufundishaji ngazi ya vilabu na licha ya kuijenga timu kwa ujumla pia anauwezo wa kumnoa mchezaji mmoja mmoja na kumfanya bora zaidi.

"Hans tulishakaa naye sana, ni kocha ambaye mwaka jana ametufundisha na kamaliza mkataba wake akaenda zake  Saudi Arabia, Tunamfahamu ni mwalimu mzuri ambaye anauwezo wa kumbadirisha mchezaji akawa katika hatua nyingine" Amemalizia Cannavaro ambaye amekabidhiwa jukumu la kushika mkoba wa timu hiyo ambao ni wawakirishi wa Tanzania katika michuanoo ya kombe la Shirikisho barani Afrika.



Comments