Na. Richard Bakana, Dar es salaam
Nahodha wa klabu ya Yanga SC pamoja na Timu ya Taifa ya Tanzania Nadir Haroub 'Cannavaro' ametoboa siri ya kufanya kwake vizuri kwenye mchezo wa Soka akidi kuwa Muziki wa Bongo Flaver ndio sababu kubwa ya mafanikio yake.
Akiongea na Shaffihdauda.com Cannavaro ambaye kwa sasa yupo nchini Botswana kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa marudiano kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika, Dhidi ya BDF XI, amesema anaposikiliza muziki wa kizazi kipya huwa anapata morali ya kufanya kazi kwa nguvu na kujitumazaidi Uwanjani.
"Nikiwa safarini huwa napenda sana kusikiliza Bongo fleva, Kwa upande mwingine nikisha sikiliza Bongo fleva huwa Napata morali ya kucheza sana mpira" Amesema Cannavaro.
Mchezaji huyo ambaye kwasasa ni roho ya Yanga katika safu ya ulinzi amesema kunawasanii wa Tanzania ambao huwa anapenda kusikiliza kazi zao kila zinapotoka pamoja na zilenyimbo ambazo zinafanya vizuri katika soko la muziki nchini.
"Kunawasanii wengi tu wananivutia, lakini mimi huwa napenda sana kumsikiliza Diamond, Ali Kiba, Kassim Mganga, Mwana FA, Charles Baba wengi sana lakini mimi huwa napenda sana kusikiliza Bongo Fleva" Amesema Nadir Haroub 'Cannavaro.
Comments
Post a Comment