CAF YAKUBALI AFCON 2023 IFANYIKE JUNI BADALA YA JANUARI




CAF YAKUBALI AFCON 2023 IFANYIKE JUNI BADALA YA JANUARI

150208181027-afcon-final2-super-169

JOHANNESBURG, Afrika Kusini
Michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) itavutwa kutoka Januari hadi Juni ili kuipisha michuano ya Kombe la Dunia 2022, Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Valcke alisema jana, Jumatano.

"Afrika imekubali mara moja haitaanda AFCON Januari 2023," Valcke aliwaambia waandishi wa habari Qatar, waandaji wa Fainali za Kombe la Dunia 2022.

"Si kwamba AFCON haitafanyika, bali wataiahirisha hadi Juni ili kutoa fursa kwa wachezaji wa Afrika kushiriki Kombe la Dunia."

Guinea, nchi ya Afrika Magharibi, ndiyo mwenyeji wa AFCON 2023.



Comments