BAYERN MUNICH YAANZA KWA SARE DHIDI YA SHAKHTAR DONETSK … Xabi Alonso atibua mchezo wake wa 100 Champions League
Xabi Alonso amejikuta akimaliza vibaya mchezo wake wa 100 wa Champions League kwa kulimwa kadi nyekundu ingawa hata hivyo haijaigharimu Bayern Munich baada ya kuambulia sare ya 0-0 ugenini kwa Shakhtar Donetsk.
Ikiwa imetoka kufanya maangamizi ya 8-0 kwa Humburg kwenye Bundesliga, Bayern ikashindwa kabisa kuonyesha makali yake kwa Shakhtar ambayo nayo ilishindwa kutumia mwaya wa kutolewa kwa Alonso kipindi cha pili.
Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool na Real Madrid alipewa kadi ya pili ya njano zikiwa zimesalia dakika 25 lakini haikubadisha kabisa sura ya mchezo uliopigwa Arena Lviv.
SHAKHTAR DONETSK (4-4-2): Pyatov; Srna, Kucher, Rakitskiy, Shevchuk; Douglas Costa (Romero Bonfim 78), Fred, Fernando, Taison (Wellington 83); Teixeira, Luiz Adriano (Gladkiy 88). Subs not used: Kanibolotskiy, Krivtsov, de Azevedo, Ilsinho
BAYERN MUNICH (3-4-3): Neuer; Rafinha, Boateng, Alaba; Alonso, Schweinsteiger, Bernat, Götze (Lewandowski 74); Robben, Müller (Badstuber 69), Ribery. Subs not used: Dante, Rode, Starke, Reina, Weiser
Comments
Post a Comment