Barcelona yasaka saini ya Mrithi wa Messi kutoka Kenya, Ni kinda wa miaka 17



agegeMohamed Nyanje 'Agege 10′ akimenyana na mabeki wa Academy ya Barcelona.

Na. Richard Bakana, Dar es salaam

Klabu ya FC Barcelona ipo kwenye mchakato wa kuwinda saini ya kinda wa Kenya ambaye anakipiga katika kituo cha kukuza vipaji cha Aspire Football for Hope Academy, nchini Qatar, Mohamed Rama Nyanje maarufu kama Messi Agege10.

Akizungumza na Shaffihdauda.com akiwa Qatar, Kinda huyo ambaye alizaliwa Desemba 24, 1998 katika eneo la Kisuani, Mombasa, Kenya, amesema kuwa Barcelona kupitia kwa wakala ambaye aliibua kipaji cha Nguli wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi, Josep Colomer, wamekuwa wakisaka kwa hudi na ubani saini ya Yoso huyo lakini uongozi wa Academy umekuwa mgumu kutoa ruhusa.

"Kweli Barcelona wananitaka na team yangu bado inakaba kuniachilia, alioniselect ndoo aliomselect messi wa barca sasa ana dai mm ni next messi na ninavo cheza ni kama leo messi alivo kuwa na umri kama wang .. ndoo maana bado ajataka kuni release, But bado wanaongea" Amesema Messi Agege ambaye ni rafiki mkubwa wa Kinda wa Tanzania, ambaye wanacheza wote timu moja Martin Tangazi.kocha

 Mohamed Nyanje (Messi Agege 10) akiwa ameshikwa kichwani na Wakala wa wachezaji aliyemuibua Lionel Messi wa Barcelona, Josep Colomer.

Messi Agege anasema kuwa, Barcelona walimuona baada ya Academy yao Aspire kushiriki mashindano ya Mediterranean lnternational cup 2014, ambayo yanahusisha Academy za vilabu vikubwa Duniani kama Real Madrid, Barcelona ambao ndio walikuwa wenyeji pamoja na timu nyingine kama Machester City.

 Katika michuano hiyo Barcelona ilijikuta ikiambulia kipigo cha bao 1-0 kitu ambacho kiliwafanya uongozi wa klabu hiyo maarufu Duniani usiridhike na matokeo hayo na kuomba mchezo wa kirafiki baada ya mashindano lakini bado Aspire wakaibuka na ushindi wa bao 2-1.

 "Barcelona tulipocheza nao, Tuliwafunga 1-0 kwenye Tournament, baada ya kumalizika walituita kwao La Masi kwa Friendly game tukawafunga 2-1, Nlikiwa best player wa tournament" Amesema Kinda huyo anayevaa jezi namba 10 mgongoni na kutumia mguu wa Kushoto kama Lionel Messi mwenyewe wa Barcelona.

 Mchezaji huyo mwenye ndoto za kuwa nyota mkubwa Duniani kupitia kipaji chake cha kucheza mpira wa miguu amesema kutokana na uwezo alionao pale katika kituo chao, Kocha wake huwa anamtumia kama namba 10 lakini muda mwingine anamuacha acheze huru katika timu zao za U17, U18, U19 na U20 licha ya yeye kuwa na umri wa miaka 17.agege 3

Shaffihdauda.com ilipomuuliza Messi Agege kuwa ni mchezaji gani katika ligi ya Tanzania bara anayemkubali zaidi, kinda huyo alimtaja mchezaji wa Bandari, Chrispine Odula, ambaye amewahi kuzichezea Coastal Union ya Tanga na Azam FC ya Jijini Dar es salaam.

"Namkubali sana chrispine odula anacheza bandari aliwai kuchezea Azam na Coastal Union, Ni mfano mzuri kwa youth player (Vijana) anapenda kutia watu morali  na hajiskii, siunajua maplayer wetu Waafrika wanapenda ukubwa, Lakini yeye anajiweka kama watu mwingine tuu"  Amesema Kijana huyo ambaye amesema anamahusiano ya kimapenzi na mwanadada Yusriyah anayeishi Dubai.10979241_657486954380246_366618948_n

Akiwa Kenya, Messi Agege huwa anapendelea vitu kama hivi, "Napenda kuwa karibu na family kwa ajili uwa nimekaa msimu mzima bila kuwa nao karibu ku enjey kama kwenda matembezi pamoja ..na mara ingine uwa na kaaa na marafiki zangu kwa ajili na feel poa sana nikitia story na wao na kucheza mechi za kirafiki mtaani".

Anamzungumziaje Mtanzania Martin Tangazi?

"Martin nafahamiana nae nikama ndugu tuu kwa kwasababu ni rafiki yangu wakaribu sana, Tunapendana sana akiwa na shida mtu wake wa kwanza ni mimi kunijulisha hata kama hatuko pamoja, Kiwango chake kiko poa sana na ni player anae taka ku improve kila siku yaani anabidii ya kujua kila jipya, Nafasi yake katika timu iko sawa sana kaka, kocha wake anamkubali maana anasaidia timu" Amesema Agege10.

agege 122Agege 10 akiwa na Bosi wa Academy ya Aspire.11004050_657501911045417_281008141_nagege 2agege 4agege 6



Comments