Azam wazipoteza fitina za Wasudan


Azam wazipoteza fitina za Wasudan
 10403629_918481188192238_6973291696561800103_n
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, Azam fc wanaendelea kujifua nchini Sudan kuelekea mechi ya marudiano dhidi ya wenyeji Al Merrick itayopigwa kesho jumamosi usiku uwanja wa Odmarman, mjini Khartoum.
Azam fc wataingia katika mechi ya kesho wakiwa na faida ya mabao 2-0 waliyovuna februari 15 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.
Mabao hayo yalifungwa na Didier Kavumbagu na Nahodha John Raphael Bocco 'Adebayor'.
 Licha ya kufanyiwa fitina za hapa na pale, kocha mkuu wa Azam, Mcameroon, Joseph Marius Omog ameendelea na programu yake ya mazoezi leo.
Azam wanahitaji sare ya aina yoyote ile au kufungwa si zaidi ya goli 1-0 ili kusonga mbele.

 



Comments