Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC wametupwa nje ya michuano ya klabu bingwa Afika baada ya kukubali kichapo cha 3-0 ugenini dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Azam imeshindwa kulinda ushindi wake wa 2-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Azam Complex jijini Dar es Salam na hivyo kuaga kwa jumla ya bao 3-2.
El Merreikh walifunga bao moja katika kipindi cha huku mawili yakija ukingoni mwa kipindi cha pili.
Mchezo huo umechezwa Jumamosi jijini Khartoum kwenye uwanja wa Merreikh kuanzia saa 2 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya Radio Uhuru, waamuzi kutoka Zambia walionekana wazi kuwabeba wenyeji.
Comments
Post a Comment