Torres (kulia) na wachezaji wake wakimzonga mwamuzi
FERNANDO Torres na wachezaji wenzake walimzonga mwamuzi wa mechi yao ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 dhidi ya Bayer Leverkusen, Pavel Kralovec kutoka Jamhuri ya Czech kufuatia kukaa goli la kichwa la mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea katika dakika ya 75′.
Leverkusen wakiwa nyumbani dimba la BayArena waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Bao hilo pekee la ushindi lilifungwa na Hakan Calhanoglu katika dakika ya 57′.
Wenyeji walicheza vizuri na walimiliki mpira kwa asilimia 64 kwa 36 za wapinzani wao.
Walipiga mashuti 5 yaliyolenga lango dhidi ya 2 ya Atletico.
Atletico wanahitaji ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya marudiano itayopigwa dimba la Vicent Calderon mjini Madrid.
Comments
Post a Comment