WAKIWA dimba la nyumbani Emirates mjini London, Asernal wamekubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Monaco ya Ufaransa katika mechi ya kwanza ya raundi ya 16 ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Geoffrey aliifungia Monaco bao la kuongoza katika dakika ya 38′, Dimitar Berbatov alitia kambani la pili dakika ya 53′.
Arsenal wakasawazisha bao la kwanza dakika ya 90′ kupitia kwa Alex Oxlade Chamberlain, lakini Yannick Ferreira-Carrasco akaifungia Monaco bao la tatu na la ushindi.
Kwa matokeo hayo, Arsenal wanahitaji ushindi wa mabao 3-0 ugenini ili kuweza kuitoa Monaco.
Takwimu za mchezo huo zinaonesha kuwa wageni walipiga mashuti 7 kwa 4 yaliyolenga lango.
Mashuti yasiyolenga lango yalikuwa 10 kwa Arsenal na 3 kwa Monaco.
Arsenal kama ilivyokawaida waliongoza kumiliki mpira kwa asilimia 55 kwa 45 za Monaco.
Comments
Post a Comment