Na Augustino Mabalwe
Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema kuwa anatamani kuwa kocha wa timu ya taifa ya italia na kuiwezesha timu hiyo kuchukua kombe la dunia.
Ancelotti mwenye umri wa miaka 55 ameshakuchukua vikombe mbalimbali akiwa na vilabu vya Juventus,AC Milan,Chelsea,Psg na Real Madrid.
Kocha huyo ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Real Madrid amesema ni ndoto zake za siku nyingi kuja kuifundisha timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba kwa muda mrefu tangu ichukue ubingwa wa dunia mwaka 2006 kule nchini Ujerumani.
"Ndoto zangu ni kuifundisha timu ya taifa ya Italia na ninaamini siku moja zitatimia,kwani lengo langu ni kuchukua ubingwa wa dunia na timu hiyo " alisema kocha huyo raia wa Italia.
Ancelotti kwa sasa anafanya vizuri akiwa na klabu ya Real Madrid na yupo kileleni katika msimamo wa ligi kuu nchini hispania huku akiwa bingwa mtetezi wa klabu bingwa barani ulaya na klabu bingwa dunia
Comments
Post a Comment