ALLY CHOCKY NA SUPER NYAMWELA TAYARI WAKO NDANI YA JAPANI …wakirejea Bongo ni Twanga Pepeta, Extra Bongo ‘yazikwa’
Mkurugenzi, mwimbaji na mtunzi wa Extra Bongo – Ally Chocky – ametua jijini Tokyo, Japan leo asubuhi na anatarajiwa kukaa huko kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Chocky ameandamana na msanii mwingine mwandamizi wa bendi hiyo Super Nyamwela ambapo wanatarajiwa kufanya maonyesho kadhaa ya muziki kwa kushirikiana na bendi ya mmoja ya mwimbaji wa Kitanzania mwenye maskani yake Japan.
Saluti5 imepewa habari za uhakika kuwa wasanii hao watakuwa huko kwa zaidi ya mwezi mmoja na mara watakaporejea Tanzania watajiunga moja kwa moja na bendi ya The African Stars Band "Twanga Pepeta".
Kwa maana hiyo ni kwamba bendi ya Extra Bongo imevunjwa rasmi japo kwa kimya kimya na tayari wanamuziki kadhaa wa bendi hiyo wamehamia bendi zingine.
Comments
Post a Comment