ZITTO KABWE AFANYA ‘KUFURU’ MALAIKA BAND MANGO GARDEN …awatia wazimu mashabiki, alizwa na wimbo “Nani Kama Mama”, maelfu ya pesa zamtoka jukwaani



ZITTO KABWE AFANYA 'KUFURU' MALAIKA BAND MANGO GARDEN …awatia wazimu mashabiki, alizwa na wimbo "Nani Kama Mama", maelfu ya pesa zamtoka jukwaani
ZITTO KABWE AFANYA 'KUFURU' MALAIKA BAND MANGO GARDEN            …awatia wazimu mashabiki, alizwa na wimbo

Hakika Ijumaa ilikuwa ni siku ya waheshimiwa kutesa kwenye viwanja vya burudani, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe naye alikuwa na yake kwenye jukwaa la Malaika Band ndani ya ukumbi wa Mango Garden.

Wakati Mbunge wa jimbo la Sikonge, Mheshimiwa Said Nkumba alitesa kwenye jukwaa la Msondo Ngoma pale Leaders Club, Zitto alifunika vibaya sana Mango Garden, alikuwa zaidi ya shabiki, alikuwa zaidi ya pedeshee, alikuwa zaidi ya mwimbaji.

Zitto alipanda jukwaani wakati Christian Bella akiimba wimbo wake wa "Nani Kama Mama",  Mheshimiwa akachotwa na hisia za wimbo huo hadi mchozi mwembamba ukamtoka (bila shaka ni kwa kumbukumbu ya msiba wa mama yake mzazi uliotokea mwaka jana), lakini baadae akaimarika na kuthubutu kuuimba wimbo huo.

Mheshimiwa Zitto akaucheza pia wimbo huo, mashabiki wakamiminika jukwaani kupiga naye picha, kwa muda wa takriban dakika 20 alizosimama jukwaani, mbunge huyo akadhihirisha kuwa ni mtu wa watu, Mango Garden 'ilisimama' kwa muda.

Kama kuna mapedeshee waliokuwepo Mango Garden, basi jana walizima ngebe zao, Zitto alifunika, alitunza pesa nyingi sana.

Christian Bella peke yake alipokea zaidi noti 50 za elfu kumi kumi kutoka kwa Zitto huku zingine zikiwa ni dola za Kimarekani. Watu wanatumia pesa bwana!

 Zitto Kabwe akishindwa kuzuia machozi
Zitto Kabwe (katikati) akiwa kwenye hisia kali
 Hakika wimbo ulimgusa sana Mheshimiwa Zitto Kabwe
 Zitto Kabwe akipiga picha na mashabiki
Mwenyekiti wa Bongo Dansi Mathew Kiongozi (mwenye shati jekundu) akimtunza Zitto Kabwe
 Wasaa wa picha ya pamoja
Ni wakati wa kunesa sasa


Comments