YAYA TOURE NAYE ATUPIA ZENGWE MANCHESTER CITY, ASEMA HANA UHAKIKA KAMA ATAKUWEPO HAPO MSIMU UJAO



YAYA TOURE NAYE ATUPIA ZENGWE MANCHESTER CITY, ASEMA HANA UHAKIKA KAMA ATAKUWEPO HAPO MSIMU UJAO

Yaya Toure has claimed that he doesn't know if he'll                be a Manchester City player next season

Yaya Toure  kwa mara nyingine tena ametoa kauli inayotishia hatma yake ndani ya Manchester City baada ya kusema kuwa hana uhakika kama atabakia katika hiyo msimu ujao.

Lakini haraka sana kocha wake Manuel Pellegrini akafuta gumzo la uhamisho kupitia mkutano wa waandishi wa habari Ijumaa na kusisitiza kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 amejizatiti klabuni.

"Sijui kama nitabakia Manchester City. City ni klabu kubwa ambayo imenifanya nivune mambo mengi sana lakini sijui nini hatma yangu," alisema mchezaji huyo bora wa Afrika kwa mara nne mfululizo.



Comments